1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroSudan

Watu milioni 5 hatarini kutumbukia kwenye baa la njaa Sudan

16 Machi 2024

Umoja wa Mataifa umetoa wito kwa pande zinazohasimiana nchini Sudan kuruhusu usafirishaji wa misaada ya kibinadamu ili kukabiliana na kile ilichokiita "janga la njaa."

https://p.dw.com/p/4dngx
Sudan Unicef
Mama mkimbizi akiwa na mtoto wake wa miezi mitatu katika kambi ya wakimbiziPicha: Nariman El-Mofty/AP Photo/picture alliance

Kulingana na waraka wa Umoja wa Mataifa ulioonekana na shirika la habari la AFP, Wasudan milioni tano wako katika hatari ya kukabiliwa na uhaba wa chakula katika miezi ijayo wakati vita kati ya jeshi la Sudan na kundi la wanamgambo la RSF bado vinaendelea.

Vita hivyo vimesababisha mzozo mbaya wa kibinadamu na uhaba mkubwa wa chakula huku nchi hiyo ikiwa ukingoni mwa baa kubwa la njaa.

Soma pia: Guterres ataka usitishaji mapigano Gaza, Sudan

Mratibu wa Umoja wa Mataifa wa misaada ya kibinadamu Martin Griffiths ametahadharisha kuwa, Wasudan milioni 18 tayari wanakabiliwa na uhaba wa chakula - kiwango hicho kikiwa rikodi wakati wa msimu wa mavuno.

Griffiths ameendelea kueleza kuwa, karibu watoto 730,000 nchini humo, ikiwa ni pamoja na zaidi ya watoto 240,000 katika jimbo la Darfur, wanaelezwa kuwa na utapiamlo mbaya.