1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN: Shambulizi la droni lamuuwa mtu mmoja Sudan

7 Februari 2026

Shambulio la droni dhidi ya msafara wa misaada katika jimbo la Kordofan Kaskazini mwa Sudan limemuua mtu mmoja na kuwajeruhi wengine kadhaa huku asasi za kiraia nchini humo zikiwalaumu wanamgambo.

https://p.dw.com/p/58Gve
Sudan El Obeid 2026 | kambi ya wakimbizi
Picha ya kambi ya wakimbizi ya El Obeid nchini SudanPicha: El Tayeb Siddig/REUTERS

Msafara huo wa jana ulikuwa unaelekea katika eneo karibu na El-Obeid, mji unaodhibitiwa na jeshi lakini ambao umekuwa ukizingirwa na vikosi vya wanamgambo wa RSF kwa mwaka mmoja.

Mratibu wa misaada kwenye Umoja wa Mataifa Denise Brown, amesema baada ya kutembelea El-Obeid kuwa alishuhudia athari za shambulizi hilo zilizojumuisha kuchomwa kwa malori ya misaada.

Alielezea wasiwasi mkubwa juu ya shambulio hilo na akatoa wito wa kuzingatia ulinzi wa wafanyakazi wa mashirika ya misaada, mali na bidhaa.

Shirika la kufuatilia haki za binadamu nchini humo liitwalo Emergency Lawyers, limethibitisha kutokea kwa shambulizi hilo na kulihusisha moja kwa moja kundi la RSF.