1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UN kutuma ujumbe kutathmini usitishwaji wa mapigano Kongo

3 Februari 2026

Ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo utapeleka timu yake ya kwanza kutathmini usitishwaji wa mapigano kati ya serikali na waasi wa AFC/M23.

https://p.dw.com/p/57yZD
Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Goma 2025 | Waasi wa M23
Waasi wa kundi la M23 wakipanda magari yao baada ya sherehe ya ufunguzi wa Caisse Generale d'epargne du Congo huko Goma, jimbo la Kivu Kaskazini Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Aprili 7, 2025Picha: Arlette Bashizi/REUTERS

Wizara ya Mambo ya Nje ya Qatar imesema hayo jana Jumatatu baada ya kuongoza mazungumzo mjini Doha na kuongeza kuwa timu hiyo itapelekwa Uvira, mji wa kimkakati mashariki mwa Kongo, ambao waasi hao waliudhibiti mwezi Disemba.

Tangazo hilo lililotolewa jana usiku ni ishara ya kupigwa hatua katika mazungumzo ya moja kwa moja yaliyoratibiwa na Doha kati ya Congo na AFC/M23, ambao mwaka uliopita walidhibiti ardhi kubwa kabisa kuwahi kuikamata Mashariki mwa taifa hilo.  

Msukumo huu wa karibuni wa kufanyia tathmini usitishwaji wa mapigano hata hivyo, unafanyika wakati mapigano yakiendelea kwenye eneo hilo la mashariki.