1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ulimwengu wapambana na nishati ya visukuku

26 Septemba 2023

Kuelekea mkutano wa mazingira wa COP28 Umoja wa Mataifa umesema bado mataifa hayajafaulu katika kudhibiti nishati ya visukuku, ambayo inaongeza joto ulimwenguni.

https://p.dw.com/p/4WpUw
Waziri wa Mambo ya Nje Ujerumani nnalena Baerbock akiwakaribisha maafisa wa serikali mbalimbali duniani katika mazungumzo juu ya hali ya hewa
Waziri wa Mambo ya Nje Ujerumani nnalena Baerbock akiwakaribisha maafisa wa serikali mbalimbali duniani katika mazungumzo juu ya hali ya hewaPicha: Tobias Schwarz/AFP/Getty Images

Imesalia miezi miwili kabla ya Mkutano wa kilele wa Mazingira wa Umoja wa Mataifa wa COP28, bado dunia iko mbali katika kuziba pengo baina ya wale wanaodai mpango wa kuachana na nishati za visukuku zinazoongeza joto ulimwenguni na mataifa yanayosisitiza kuendelea na matumizi nishati hizo. 

Mkutano wa COP28 utakaofanyika Dubai kati ya Novemba 30 na Desemba 12 unaonekana kama fursa muhimu kwa serikali za mataifa duniani kuharakisha hatua za kupunguza ongezeko la, lakini bado kuna mgawanyiko mkubwa juu ya siku zijazo katika athari ya kisukuku.

Mkutano ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mwishoni mwa wiki uliibua tena  mjadala wa muda mrefu, huku mataifa yanayokabiliwa na athari mbaya za mabadiliko ya tabianchi, kama vile Visiwa vya Marshall, yakiyaomba mataifa tajiri kuachana na nishati zinazochafua mazingira na kuwekeza katika njia mbadala.

Soma pia:Wanaharakati wa mazingira kuendeleza maandamano leo

Akizungumza katika mkutano wa kilele wa tabianchi uliofanyika sambamba na mkutano wa baraza kuu, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alisema "binaadamu wamefungua milango ya kuzimu."

Kauli hiyo ikitafsiriwa na wanamazingira kwamba alikosowa ulafi wa watu walio na maslahi katika matumizi ya nishati za visukuku.

Nchi nyingine zinazotowa au kutegemea nishati ya kisukuku zimesisitiza uwezekano wa matumizi ya teknolojia ili "kupunguza" uchafuzi, lakini wakiwa na maana ya kudhibiti tu utowaji wa nisahti hizo, badala ya kukomesha kabisa matumizi yake.

China haijaonesha nia ya kuachana na visukuku

China, mtumiaji mkubwa zaidi wa nishati za visukuku duniani, ni miongoni mwa nchi zinazoashiria kwamba zitaendelea kutumia kwa miongo kadhaa.

Marekani imesema inaunga mkono hatua ya kuondolewa kwa nishari za visukuku huku ikikubali kwamba kuna mipango ya baadhi ya nchi zinazoendelea kuwekeza katika nishati hizo.

Waziri wa Mambo ya Nje China  Li Qiang akiwa na Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya, Ursula von der Leyen
Waziri wa Mambo ya Nje China Li Qiang akiwa na Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya, Ursula von der LeyenPicha: imago images

Ingawa mjumbe wa mabadiliko ya tabianchi wa Marekani, John Kerry, amehoji ikiwa teknolojia ya kudhibiti utowaji wa hewa chafu inaweza kupatikana kwa haraka.

Umoja wa Ulaya na mataifa mengine yanayopigania nishati salama kwa mazingira wanasema ni muhimu kuongoza kwa sera na uwekezaji uliojitenga mbali na nishati zinazochafua hali ya hewa.

Soma pia:Mawaziri wa G7 waahidi kuachana na mafuta ya visukuku

Lakini kwa kuzingatia mgawanyiko uliopo juu ya mustakabali wa nishati za visukuku, huku zaidi ya nchi 80 zikijaribu bila mafanikiokufikia makubaliano katika mkutano wa kilele wa COP27 mwaka jana.

Wapatanishi sasa wanatafuta misamiati mipya katika kutafuta maelewano.

Katika kile kilichoonekana kama mafanikio yanayowezekana mnamo Aprili,
kundi la mataifa saba yaliyoendelea kiviwanda duniani, G7, yalikubali kuharakisha kile walichokitaja mchakato wa kuondoa mafuta yasiyobadilishwa.

Kwa kutumia msamiati wa "yasiyobadilishwa", ahadi hii ililenga mafuta yaliyotumika bila ya kutumia teknolojia ya kupunguza hewa chafu.

Lakini kufikia Julai, ahadi hiyo iliyumba wakati kundi la G20 ambalo linajumuisha watowaji wa mafuta na gesi kama Saudi Arabia na Urusi liliposhindwa kufikia muafaka juu ya suala hilo.

Mkwamo uko wapi kuondoa nishati ya visukuku?

Waziri wa Mabadiliko ya Tabianchi wa Ireland, Eamon Ryan, amesema suala la kuondoa mafuta yote ya visukuku au utengenezaji wake linaweza kuwa gumu zaidi katika mkutano wa COP28.

Kundi la nchi 17 - zikiwemo Ufaransa, Kenya, Chile, Colombia na mataifa ya visiwa vya Pasifiki ya Tuvalu na Vanuatu - wiki iliyopita lilitoa wito wa kuondolewa kwa mafuta ambayo yanazuiamatumizi ya teknolojia ya kuondosha hewa chafu kwenye tabakahewa.

Mradi wa kupambana na mabadiliko ya tabia nchi Rwanda

Soma pia:Kenya kuwapa fidia waathirika wa mabadiliko ya tabianchi

Makampuni yanayozalisha mafuta na gesi yanasema dunia itahitaji teknolojia ya kupunguza uchafuzi ili kuwezesha uzalishaji zaidi wa nishati wenye uchafuzi mdogo.

Lakini baadhi ya nchi zinazoendelea pia zinazopinga kuondolewa kwa nishati za visukuku zinasema zinahitaji nishatihiyo ili kuongeza uzalishaji wa umeme katika kuboresha maendeleo ya kiuchumi kwa njia sawa kama Japan na Marekani.

Ndani ya Umoja wa Afrika, baadhi ya serikali zimeshutumu nchi za Magharibi kwa unafiki kwa kutumia hoja za kuhifadhi hali ya hewa kukataa kufadhili miradi ya gesi katika mataifa yanayoendelea, wakati wakiendelea kuchoma gesikwenye mataifa yao.