Umwagaji damu waendelea Syria | Matukio ya Kisiasa | DW | 19.11.2011
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Umwagaji damu waendelea Syria

Mzozo wa Syria unaendelea kusababisha umwagaji damu nchini humo, licha ya Umoja wa Nchi za Kiarabu kuitaka serikali ya Rais Bashar al-Assad kuacha kutumia mabavu dhidi ya waandamanaji.

epa02941263 Syrians shout pro-Syrian regime slogans during a sit in staged before the offices of the European Union in Damascus, Syria, on 29 September 2011. According to local sources, the protest aimed at showing support with Syrian Addounia TV channel, that was recently hit by EU sanctions. The European Union on 23 September has extended its sanctions against Syria to include six Syrian companies, including Addounia TV, to intensify pressure on Assad, who has come under withering international criticism for his regime's crackdown on protests. EPA/YOUSSEF BADAWI +++(c) dpa - Bildfunk+++

Syria yaendelea kutumia nguvu dhidi ya waandamanaji

Siku ya Ijumaa raia 12 waliuawa na vikosi vya usalama vya Syria. Watoto 2 ni miongoni mwa wahanga hao.Mauaji hayo yametokea wakati Uturuki na Marekani zikionya juu ya hatari ya vita vya wenyewe kwa wenyewe kuibuka nchini Syria na huku maelfu ya watu wakiandamana barabarani bila ya kuvijali vikosi vya usalama vilivyosambazwa kwa wingi na kutoa mito ya kuwafukuza mabalozi wa Syria.

Uturuki imetahadharisha juu ya uwezekano wa vita vya wenyewe kwa wenyewe kutokea wakati idadi ya wanajeshi wanaouawa na wenzao walioasi ikiongezeka. Onyo hilo pia limetolewa na wachambuzi wanaoyafuatiliza matukio ya nchini Syria inayozidi kutengwa kimataifa. Umoja wa Nchi za Kiarabu umeitaka Syria isitishe umwagaji damu wa waandamanaji, ifikapo usiku wa manane wa Jumapili ama sivyo itakabiliwa na hatari ya kuwekewa vikwazo. Uanachama wake katika Umoja wa Nchi za Kiarabu wenye mataifa 22 umesitishwa kwa muda.

The empty chair of the Syrian delegate is seen at the Arab League foreign ministers meeting in Rabat, Morocco Wednesday, Nov. 16, 2011. Foreign ministers from the 22-member Arab League on Wednesday are expected to formalize their weekend decision to suspend Syria for refusing to end its bloody crackdown against anti-government protesters. Inscription reads: Arab Republic of Syria. (Foto:Abdeljalil Bounhar/AP/dapd)

Kiti kitupu cha mjumbe wa Syria kwenye mkutano wa mawaziri wa nje wa Umoja wa Nchi za Kiarabu mjini Rabat,Morocco

Kwa upande mwingine, Iran imesema, hatua hiyo ni "kosa la kihistoria" na kwamba hatua hiyo ndio itakayosababisha vita vya wenyewe kwa wenyewe. Kwa tathmini ya Umoja wa Mataifa, hatua za ukandamizaji zinazochukuliwa na serikali ya Syria kuyazima maandamano yaliyoibuka katikati ya mwezi Machi, zimesababisha vifo vya zaidi ya watu 3,500.

Hapo mwanzoni, waandamanaji walimiminika barabarani kudai demokrasia katika nchi hiyo ya kiarabu inayotawalwa kwa mabavu, lakini sasa watu hao wanataka kuitimua madarakani serikali ya Rais Assad na wanaungwa mkono na wengi katika ulimwengu wa magharibi.

Mwandishi,Martin,Prema/afpe

Mhariri: Sekione Kitojo

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com