1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umwagaji damu waendelea nchini Kenya

4 Februari 2008
https://p.dw.com/p/D1rp

NAIROBI:

Si chini ya watu 70 wameuawa nchini Kenya katika machafuko ya kikabila yaliyotokea mwishoni mwa juma.Kiongozi wa upinzani Raila Odinga ametoa mwito kuwa Umoja wa Afrika au Umoja wa Mataifa upeleke Kenya vikosi vya amani ili kusaidia kukomesha machafuko ya kikabila.Akaongezea kuwa yeye na wafuasi wake hawaamini tena kwamba vikosi vya serikali havina upendeleo.

Licha ya makubaliano ya amani yaliyosimamiwa na Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan,umwagaji damu wa kikabila unaendelea nchini Kenya.Si chini ya watu 900 wameuawa tangu kufanywa uchaguzi wa rais uliozusha mabishano.Odinga na wafuasi wake wanasema,uchaguzi huo umefanyiwa udanganyifu.