Umoja wa Ulaya watafuta suluhisho la mzozo wa madeni | Matukio ya Kisiasa | DW | 26.10.2011
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Umoja wa Ulaya watafuta suluhisho la mzozo wa madeni

Jitahada za kutafuta ufumbuzi wa mzozo wa madeni katika kanda inayotumia sarafu ya euro zinaendelea. Baadae leo hii viongozi wa Umoja wa Ulaya watakutana mjini Brussels katika mlolongo wa mikutano ya umoja huo.

FILE - In this Sept. 2, 2009 file picture the Euro sculpture is see in front of the European Central Bank ECB in Frankfurt, central Germany. Alarmed by the risk to the euro, the European Central Bank exercised what analysts called its nuclear option early Monday May 10, 2010 , announcing it would intervene in bond markets as part of the wider effort to protect the eurozone. The central bank for the 16 countries that use the euro said its move was designed to ensure depth and liquidity in those market segments which are dysfunctional. The announcement was part of a decision by the European Union and International Monetary, who pledged nearly US dlrs 1 trillion to defend the euro and the eurozone. (AP Photo/Michael Probst, File)

Benki Kuu ya Umoja wa Ulaya

Viongozi hao wanatazamiwa kuashiria kuwa ikihitajika, watakuwa tayari kuimarisha mitaji ya baadhi ya benki ili kurejesha imani katika masoko ya fedha. Katika mswada wa taarifa, iliyotolewa kabla ya mkutano wa jioni ya leo mjini Brussels, viongozi wa Umoja wa Ulaya wameashiria kuwa wapo tayari kuzidhamini benki zinazohitaji msaada. Ahadi hiyo inasisitiza azma ya serikali za nchi wanachama, kuzuia matatizo ya fedha yatakayoweza kuhatarisha uchumi katika kanda hiyo. Katika mswada huo, viongozi wa Umoja wa Ulaya wamesisitiza umuhimu wa kurejesha imani katika sekta ya benki.

Mario Draghi atakaekuwa kiongozi mpya wa Benki Kuu ya Ulaya, amesema, benki kuu katika kanda ya euro, zimeazimia kuchukua hatua za kipekee ili kuzuia vurugu katika masoko ya fedha yanayokwamisha biashara za fedha. Hata hivyo, Draghi atakaemrithi Jean-Claude Trichet tarehe mosi Novemba, alieleza kinagaubaga kuwa hizo ni hatua za mpito. Amesema, ni wajibu wa serikali husika, kushughulikia kiini cha mzozo wa madeni ulioanza miaka miwili iliyopita nchini Ugiriki.

Bundeskanzlerin Angela Merkel (CDU) unterhaelt sich am Mittwoch (19.10.11) in der Alten Oper in Frankfurt am Main bei der Verabschiedungsfeier fuer Jean-Claude Trichet, dem scheidenden Praesidenten der Europaeischen Zentralbank (EZB), mit Trichet. Trichet ist seit 2003 Praesident der EZB, seine Amtszeit endet am 31. Oktober 2011. (zu dapd-Text) Foto: Arne Dedert/Pool/dapd

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel(kushoto) katika sherehe ya kumuaga Rais wa Benki Kuu ya Ulaya, Jean-Claude Trichet

Wakati huo huo, Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel, alieungwa mkono kwa wingi mkubwa bungeni mjini Berlin, kuimarisha uwezo wa mfuko wa kuzinusuru nchi zenye matatizo katika kanda ya euro amesema, lengo ni kupunguza deni la serikali ya Ugiriki hadi asilimia 120 ya pato lake jumla la mwaka, ifikapo mwaka 2020. Hapo kabla alisema:

"Serikali kuu inataka umoja wa kiuchumi na sarafu utakaoleta utulivu. Ndio maana mbali na kuitatua migogoro sugu, tunabidi tuchukue hatua za kinga kwa siku ziijazo, kwa kuwepo jukumu la pamoja miongoni mwa nchi wanachama katika kanda ya euro."

Katika hotuba yake bungeni, alisema, Ujerumani na Ulaya zinakodolewa macho na ulimwengu mzima, kutazama kama wapo tayari na wanaweza kuwajibika. Kura iliyomuunga mkono Merkel, imeimarisha mamlaka yake katika majadiliano yatakayofanywa jioni ya leo mjini Brussels. Viongozi wa Umoja wa Ulaya watajaribu kukubaliana njia mbali mbali za kuutanzua mzozo wa madeni wa kanda ya euro unaozidi kuwa mkubwa. Lakini kuna shaka iwapo makubaliano kamili yatapatikana leo hii, kwani bado kuna tofauti za maoni katika masuala mengi yaliyo muhimu. Hata hivyo, moja ni dhahiri, suala la kusamehe sehemu ya madeni ya Ugiriki halitoepukwa tena. Lakini kile wanachotaka kujua wamiliki wa dhamana za serikali ya Ugiriki, ni kiwango cha madeni kitakachopunguzwa.

Mwandishi: Martin,Prema/rtre

Mhariri: Othman, Miraji

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com