1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Ulaya walaani shambulio la al-Shabaab

25 Agosti 2010

Mkuu wa sera za kigeni wa Umoja wa Ulaya, Bibi Catherine Ashton amelaani shambulio la wanamgambo lililouwa watu 31 katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu siku ya Jumanne.

https://p.dw.com/p/OvJu
Somali government forces walk outside the Muna Hotel in Mogadishu, Somalia, Tuesday Aug, 24, 2010. A suicide bomber and a gunman stormed the hotel in Somalia's capital on Tuesday, killing at least 15 people, including members of parliament, a military spokesman said. (AP Photo/Farah Abdi Warsameh)
Muna Hotel iliyovamiwa na wanamgambo wa al-Shabaab mjini Mogadishu.Picha: AP

Katika shambulio hilo,wanamgambo wa kundi la al-Shabaab waliovaa sare ya jeshi la serikali,walivamia hoteli moja na walipambana na vikosi vya usalama kwa saa nzima kabla ya kuripua mabomu.

FILE - A file picture dated on Jan. 31, 2009 shows European Commissioner for Trade Britian's Catherine Ashton, speaking during a panel session at the Annual Meeting of the World Economic Forum, WEF, in Davos, Switzerland. The EU's 27 leaders were meeting Thursday Nov. 19, 2009 to try to agree on naming a first full-time president and new foreign policy chief. The EU's socialist governments have agreed to back the candidacy of the EU trade commissioner, Catherine Ashton, to become the bloc's new foreign policy chief. (AP Photo/ Keystone/Laurent Gillieron
Mkuu wa sera za nje wa Umoja wa Ulaya, Catherine Ashton.Picha: AP

Ashton amesema, Umoja wa Ulaya unashikamana na umma wa Somalia na utaendelea kuisaidia serikali ya mpito ya nchi hiyo.

Hata Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na maafisa wa serikali ya Marekani wamelaani vikali shambulio la wanamgambo hao wa Kisomali. Shambulio hilo limetokea siku ya pili ya mapigano makali yaliyozuka mjini Mogadishu ambayo hadi sasa yamesababisha vifo vya watu 70.

Mwandishi: P.Martin/ZPR