1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Ulaya wakutana na China

20 Septemba 2012

Mkutano baina ya Waziri mkuu wa China Wen Jiabao na viongozi wa juu wa Umoja wa Ulaya umefunguliwa hii leo (20.09.2012) mjini Brussels huku ajenda kubwa ikiwa ni mahusiano ya kibiashara baina ya pande hizo mbili.

https://p.dw.com/p/16BqQ
Waziri Mkuu wa China, Wen Jiabao (kushoto) akisalimiana na Rais wa Kamisheni ya Ulaya, Jose Manuel Barosso.
Waziri Mkuu wa China, Wen Jiabao (kushoto) akisalimiana na Rais wa Kamisheni ya Ulaya, Jose Manuel Barosso.Picha: dapd

Katika ufunguzi wa mkutano huo, Waziri Mkuu wa China Wen Jiabao ameelezea masikitiko yake kwa Umoja wa Ulaya kukataa kuipatia hadhi kamili ya soko pamoja na kuondoa vikwazo vya silaha.

''Tumekuwa tukifanya kazi kwa bidii kwa miaka kumi lakini ufumbuzi umekuwa ndoto. Ninasikitika sana kwa hili,'' Wen aliwaambia viongozi wa Umoja huo. Kwa maneno mengine China inataka Umoja wa Ulaya uonyeshe jitihada zaidi.

Vikwazo vya Umoja wa Ulaya kwa China viliwekwa kutokana na ukandamizaji uliofanywa wakati wa maandamano ya kudai demokrasia katika uwanja wa Tiananmen mjini Beijing mwaka 1989. China inataka vikwazo hivyo sasa viondolewe.

Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya, Jose Manuel Barroso, amesema huu ni mkutano unaotathimini maendeleo ya ushirikiano wao katika miaka 10 iliyopita.

Usalama na Amani sehemu ya ajenda

China imekuwa mshirika mkubwa wa kibiashara katika nchi za Ulaya kutokana na uchumi wake kuendelea kuimarika kutokana na unafuu wa bidhaa zinazotengenezwa nchini humo.

Rais wa Kamisheni ya Ulaya, Jose Manuel Barroso (kulia), akizungumza na Rais wa Baraza la Ulaya, Herman Van Rompuy.
Rais wa Kamisheni ya Ulaya, Jose Manuel Barroso (kulia), akizungumza na Rais wa Baraza la Ulaya, Herman Van Rompuy.Picha: dapd

Mkutano huo pia utajikita katika masuala yanayotishia amani na usalama katika ngazi ya kitaifa na kimataifa yakiwemo machafuko nchini Syria na mgogoro wa kugombea visiwa visivyokaliwa katika eneo la mashariki mwa bahari ya China baina ya China na Japan.

''Ni katika urafiki ndio maana tunaweza kujadiliana haya , yapo amabyo tunakubaliana na mengine siku zote hatukabaliani',' amesema Barroso, aliyeongeza kwamba katika kipindi chote hicho kumekuwa na ongezeko la mahausiano ya kibiashara katika utengenezaji wa bidhaa na utoaji wa huduma mbalimbali.

Kwa mwaka 2011 pekee biashara baina ya pande hizo mbili iliimarika na kufikia euro bilioni 428 ikiwa ni mara mbili tangu mwaka 2003. Umoja wa Ulaya wenye nguvu aza kiuchumi duniani na China inayoshika nafasi ya tatu, pia zitazungumzia mkatati wa ushirikiano wao na hali ya kiuchumi nchini China na katika kanda ya nchi zinazotumia sarafu ya euro, ambalo ni soko kubwa kwa China.

Waziri Mkuu wa China, Wen Jiabao, Rais wa Kamisheni ya Ulaya, Jose Manuel Barroso, na Rais wa Baraza la Ulaya Herman Van Rompuy.
Waziri Mkuu wa China, Wen Jiabao, Rais wa Kamisheni ya Ulaya, Jose Manuel Barroso, na Rais wa Baraza la Ulaya Herman Van Rompuy.Picha: dapd

Hata hivyo kumekuwa na hali ya kutoelewana katika baadhi ya maeneo mfano hivi karibuni umoja wa ulaya umeishutumu China kwa kuuza vifaa vya nishati ya jua kwa bei ya chini katika soko la Ulaya.

Awali mkutano huo uliwazuwia waandishi wa habari kumuuliza Waziri Mkuu Wen Jiabao.

Mbali na ajenda hizo za mahusiano ya kibiashara viongozi wa umoja wa ulaya wanatumia fursa hiyo kumuaga, Waziri Mkuu Wen ambaye atamaliza muda wake madarakani baadaye mwaka huu.

Mwandishi: Sylvia Mwehozi/AFP/Reuters
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman