1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Ulaya waitaka China kufungua masoko yake

Grace Kabogo
18 Septemba 2020

Ondoeni vikwazo vyenu, myafungue masoko yenu, muheshimu haki za jamii za watu wachache na muachane na ukandamizaji Hong Kong!

https://p.dw.com/p/3ifJo

Huo ndiyo ujumbe wa Umoja wa Ulaya kwa viongozi wa China kufuatia mkutano wa kilele uliofanyika kwa njia ya video kati ya pande hizo mbili. Hii ndiyo mada yetu katika kipindi cha Maoni mbele za Meza ya duara leo ambapo tutadadavua kwa kina masuala muhimu yaliyojitokeza katika mkutano huo, yakiwemo pia masuala ya mazingira. Josephat Charo ndiyo mweyekiti kwa leo akiwa na wageni Ahmed Rajab kutoka jijini London nchini Uingereza, mchambuzi wa siasa za kimataifa, huko Washington DC, Marekani tunaye Profesa Nicholas Boaz. Dar es Salaam, jiji kubwa kabisa la kibiashara la Tanzania, yuko Dr. Bravious Kyahoza, mchambuzi wa masuala ya uchumi na katika studio yetu hapa Bonn, tuko naye mstaafu Abdu Mtulya.