1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Ulaya waahidi kupeleka wanajeshi Afrika ya Kati

20 Januari 2014

Mawaziri wa mambo ya kigeni wa Umoja wa Ulaya wamekubaliana leo(20.01.2014) kutuma wanajeshi kusaidia kuimarisha usalama katika jamhuri ya Afrika ya kati.

https://p.dw.com/p/1Atri
Belgien EU-Außenministertreffen in Brüssel, 20.01.2014
Mkuu wa sera za mambo ya kigeni wa Umoja wa Ulaya Catherine Ashton(shoto)Picha: picture-alliance/dpa

Hii ni opereresheni ya kwanza kubwa ya Umoja wa Ulaya katika miaka sita iliyopita.

Pia wafadhili wa kimataifa wataipatia nchi hiyo kiasi cha dola milioni 500 mwaka huu kusaidia ujenzi mpya baada ya miezi kadha ya vita vya kimadhehebu.

Mawaziri wa mambo ya kigeni wa Umoja wa Ulaya wanaokutana mjini Brussels wameidhinisha mpango wa kutuma kikosi cha wanajeshi katika jamhuri ya Afrika ya kati nchi ambayo imeathirika na vita lakini mipango kamili kuhusu kikosi hicho bado haijafanyiwa kazi.

Aussenminister Frank-Walter Steinmeier Porträt
Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Frank-Walter SteinmeierPicha: Getty Images

Maafisa wa Umoja wa Ulaya wanamatumaini ya kuidhinishwa kwa jeshi hilo na baraza la usalama la Umoja wa Mataifa wiki hii na kwamba jeshi hilo litaanza kuwasili nchini humo ifikapo mwishoni mwa mwezi ujao. Jeshi hilo litakuwa na kituo chake katika mji mkuu wa nchi hiyo Bangui.

Nchi zitakazochangia wanajeshi

Haifahamiki ni nchi gani za Umoja wa Ulaya ambazo zitachangia wanajeshi katika kikosi hicho . Estonia imeahidi wanajeshi, na Lithuania, Slovenia, Finland, Ubelgiji, Poland na Sweden ni miongoni mwa nchi zinazofikiria kutuma wanajeshi wao katika kikosi hicho.

Nchi kubwa za Umoja wa Ulaya kama Uingereza , Ujerumani na Italia zimesema hatitatuma wanajeshi wake katika kikosi hicho. Akizungumza kabla ya kuanza mkutano huo waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Frank Walter Steinmeier amesema Ujerumani imekuwa ikitoa msaada katika bara la Afrika hususan nchini Mali.

Zentralafrikanische Republik Französische Truppen
Wanajeshi wa Ufaransa Jamhuri ya Afrika ya katiPicha: Getty Images/AFP/Miguel Medina

"Tumetoa usaidizi nchini Mali , hali imeimarika lakini bado hakuna suluhisho. Kwa hiyo kuna sababu za msingi kwamba ujumbe ulioko Mali unapaswa kuendelea, ili kuendeleza hali ya utulivu. Na hapa nina maana kwamba tunataka kutoa msaada zaidi, ikiwa ni pamoja na jamhuri ya Afrika ya kati."

Jamhuri ya Afrika ya kati ilitumbikia katika machafuko baada ya kundi la muungano wa waasi ambao wengi wao ni Waislamu , Seleka kukamata madaraka Machi mwaka jana, na kuzusha wimbi la mauaji na uporaji na kundi la waasi wa Kikristo nalo likaanza kupambana na kundi hilo baada ya kuingia madarakani rais Michel Djotodia ambaye ni Muislamu wa kwanza kushika madaraka nchini humo.

Viongozi wa kidini

Kumekuwa na mapigano ya kimadhehebu ambapo watu saba wameuwawa siku ya Ijumaa katika mapigano kati ya Wakristo na Waislamu katika mji wa Boali.

Akizungumzia suala hilo mratibu wa misaada ya kiutu wa Umoja ametaja juu ya umuhimu wa mchango wa viongozi wa kidini kwa ajili ya amani.

"Tumeona jinsi viongozi wa kidini na jamii wakijaribu kuja pamoja kupambana na jinsi ghasia hizi zinavyozidi kuwa mbaya zaidi."

Zentralafrikanische Republik Ausschreitungen Gewalt Christen Muslime 16.01.14
Wanamgambo wa Kikristo katika jamhuri ya Afrika ya katiPicha: picture-alliance/AP

Wakati huo huo wafadhili wa kimataifa wataipatia Jamhuri ya Afrika ya kati kiasi cha dola milioni 500 ili kuisaidia nchi hiyo kurejea katika hali ya kawaida baada ya machafuko ya kimadhehebu. Mataifa fadhili yanajaribu kusaidia kumaliza ghasia hizo, ambazo zimepuuziwa kwa muda mrefu.

Kamishna wa misaada ya kimataifa wa Umoja wa Ulaya Kristina Georgieva amesema baada ya mkutano ulioandaliwa na Umoja wa Ulaya na Umoja wa Mataifa mjini Brussels.

Mwandishi: Sekione Kitojo / afpe / rtre

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman