1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Ulaya na Urussi waanza mazungumzo ya ushirikiano

28 Juni 2008

-

https://p.dw.com/p/ESIb

MOSCOW

Urussi na Umoja wa Ulaya wameanzisha rasmi hapo jana mazungumzo yao yaliyocheleweshwa kwa muda mrefu juu ya kuwa na ushirikiano mpya wa kimkakati.Pande hizo mbili zilizota taarifa katika mkutano wake wa kilele huko Siberia.Rais wa Urussi Dmitry Medvedev na mwenyekiti wa tume ya Umoja wa Ulaya Jose Manuel Barosso wameitaja hatua hiyo kuwa inafungua ukurasa mpya katika uhusiano kati ya pande hizo mbili.Chini ya utawala wa rais Vladmir Putin uhusiano kati ya Urussi na Umoja wa Ulaya haukuwa mzuri kutokana na wasiwasi wa Umoja wa Ulaya juu ya nguvu za Urussi katika soko la Nishati barani Ulaya.