1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Ulaya kutuma ujumbe wake Armenia

Sudi Mnette
7 Oktoba 2022

Ulaya kutuma Ujumbe wake kwa lengo la kutatua mzozo wa Armenia na Azerbaijan na tofuti kati ya Uturuki na Sweden katika jitahada ya kujiunga na Jumuiya ya Kujihami ya NATO katika mkutano wa Jumuiya ya Kisiasa ya Ulaya.

https://p.dw.com/p/4HsJm
Tschechien, Prag | Gipfeltreffen von 44 Ländern
Picha: Petr David Josek/AP/picture alliance

Umoja wa Ulaya utatuma "ujumbe wa kiraia wa Umoja wa Ulaya" huko Armenia kusaidia mzozo wa kimipaka na jirani yake  Azerbaijan. Ujumbe huo utaanza kazi mwezi Oktoba na kuhudumua kwa takribani miezi miwili.

Taarifa ya pamoja inasema lengo la ujumbe huo ni kujenga imani na kutoa mchango wake katika kamisheni za mipaka. Taarfa hiyo imetolewa baada ya mazungumzo katika ya Waziri Mkuu wa Armenia Nikol Pashinyan, Rais wa Azerbaijani Ilham Aliyev, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron pamoja na Rais wa Baraza la Umoja wa Ulaya Charles Michel.

Armenia na Azerbaijan zimethibitisha kutimiza matakwa ya kimataifa

Tschechien, Prag | Gipfeltreffen von 44 Ländern
Kansela Olaf Scholz akiwasili PraguePicha: Sean Gallup/Getty Images

Vingozi hao watatu pamoja na rais wa baraza la Ulaya wamekutana katika nyakati kadhaa tofauti usiku wa kuamkia leo, ikiwa kandoni mwa  kile kinachofahamika kama mkutano wa Jumuiya ya Kisiasa ya Ulaya. Wamesema pia Armenia na Azerbaijan zimethibitisha kutimiza sheria ya kimataifa kwa utambuzi wa uadilifu wa eneo na uhuru wa kila upande.

Na suala la la uvamizi wa Urusi kwa Ukraine kadhalika liliingia katika mjadala wa mkutano wa Prague ambao Rais Macron alisema "Ujumbe wa kwanza mzito ambao tunataka kuuwasilisha ni kwamba tumeonyesha umoja wa nchi 44 za Ulaya ambazo zote zimesema wazi kwamba tunalaani uchokozi wa Urusi na tunaunga mkono Ukraine. Hilo linabeba dhima kubwa una tunajua kuwa Ulaya imegawanyika kwa namna fulani, lakini kwa hili tumeungana."

Erdogan aitishia Sweden katika kuiunga na NATO

Katika hatua nyingine Rais Tayyip Erdogan wa Uturuki amesema taifa lake litandedlea kuipinda Swedena katika jitihada yake ya kuomba uanachama wa NATO hadi matakwa yake yatimizwena taifa hilo, dhidi ya msimamo wake kuhusu makundi ya kigaidi. Akizungumza na waandishi wa habari kandoni mwa mkutano wa Jumuiya ya Kisiasa ya Ulaya wa Prague alisema makundi ya kigaidi yanapata nafasi huru katika taifa hilo, na wanauwakilisha katia bunge lao, ombi la Sweden halitakuwa na wepesi.

Mwezi Mei Sweden na Finland na ziliwasilisha maombi ya kujiunga na NATO, katika kile kinachoonekana hofu iliyosababishwa na kitendo cha Urusi kuivamia Ukraine. Na mombi yao yanaweza kuridhiwa kwa matakwa ya mataifa yote wanachama wa jumuiya hiyo.

Serikali ya Uturuki inayoshutumu mataifa yote hayo mawali, kwa kuwaunga mkono wapiganaji wa Kikurd, pamoja na kundi la mfuasi wa kiongozi wa kidini mwenye maskani yake nchini Marekani, Fethullah Gülen, ambayo  yote kwa pamoja Uturuki inayatazama kama makundi ya kigaidi.

Vyanzo AFP/DPA