1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Umoja wa Mataifa wakaribisha makubaliano ya Congo na Rwanda

22 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CQG5

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeyakaribisha makubaliano yaliosainiwa kati ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na Rwanda kwa lengo la kuyatimuwa makundi ya wapiganaji yasio halali kutoka mashariki mwa Congo.

Nchi wanachama wa baraza hilo wameyaelezea makubaliano hayo ya tarehe 9 mwezi wa Novemba kuwapokonya silaha waasi wa KIhutu wa Rwanda walioko Congo kuwa ni hatua muhimu kuelekea ufumbuzi wa kudumu.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limesema kuwepo kwa waasi wa Kihutu na makundi mengine ya wapiganaji kunaleta tishio kwa utulivu wa eneo hilo hata baada ya kumalizika kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Congo hapo mwaka 2003.