Umoja wa mataifa, New York. Mazungumzo juu ya Kosovo yakwama. | Habari za Ulimwengu | DW | 11.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Umoja wa mataifa, New York. Mazungumzo juu ya Kosovo yakwama.

Mjumbe wa umoja wa mataifa Martti Ahtisaari amesema kuwa mazungumzo kati ya viongozi wa Serbia na Albania kuhusiana na mpango wa umoja wa mataifa katika jimbo la Kosovo yamemalizika kwa mkwamo.

Mapendekezo, yaliyotolewa February yanalengo la kupatia ufumbuzi masuala muhimu kufuatia kuvunjika kwa iliyokuwa Yugoslavia ya zamani katika miaka ya 1990 na kusababisha mapigano.

Yaliidhinishwa na viongozi wa asili ya Albania lakini yalikataliwa na maafisa wa Serbia.

Mkutano huo ulifanyika mjini Vienna umefikisha mwisho miezi 14 ya majadiliano. Ahtisaari amesema atatuma mapendekezo yake ya kuipatia Kosovo njia kuelekea kuwa huru katika baraza la usalama la umoja wa mataifa mwezi huu.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com