Umoja wa Mataifa kujenga makaazi ukanda wa Gaza yakiratibishwa na Israel | Redio | DW | 22.03.2010
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Redio

Umoja wa Mataifa kujenga makaazi ukanda wa Gaza yakiratibishwa na Israel

Netanyahu kukutana na Rais Obama kwa mazungumzo.

Wawakilishi wa kundi la pande nne linalotafuta amani mashariki ya kati, mjini Moscow wiki iliyopita.

Wawakilishi wa kundi la pande nne linalotafuta amani mashariki ya kati, mjini Moscow wiki iliyopita.

Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia ujenzi wa makaazi katika ukanda wa Gaza linatarajia kwamba mradi wa kujenga makaazi katikia eneo hilo ukiratibishwa na Israel, basi huenda jitihada za ujenzi zikafufuliwa katika eneo hilo linalodhibitiwa na kundi la Hamas.

Makaazi mapya katika ukanda wa Gaza yataweza kusaidia takriban familia 150 na itakuwa thibitisho kwa Israel kwamba Shirika hilo la Umoja wa Mataifa linalosimia ujenzi litaweza kuendeleza ujenzi bila ya pembejeo za ujenzi kuingia katika mikono ya Hamas na makundi mengine.

Joseph Biden und Benjamin Netanyahu Flash-Galerie

Biden (kushoto) na Netanyahu katika ziara nchini Israel Machi 9 2010.

Munir Manneh ambaye ni mkuu wa ujenzi katika eneo la Gaza linaloendelezwa na kitengo cha ujenzi na ukarabati cha Umoja wa Mataifa amesema makadirio yao ni sahihi kwa sababu hawataki kulaumiwa na Israel kwa kuongeza chumvi.

Kitengo hicho cha Umoja wa Mataifa tayari kimeanza mradi wa ujenzi na ikiwa Israel itaratibisha mradi huo, basi utakuwa mkubwa zaidi tangu kusitishwa kwa vita katika ukanda wa Gaza mwaka wa 2008 vilivyodumu kwa siku 22.

Mwaka wa 2007 Israel ilipiga marufuku usafirishaji wa pembejeo za ujenzi kwa kuziba eneo la Gaza ikihofia kwamba wanachama wa Hamas wangetumia fursa hiyo kujenga kambi ya kijeshi.

Shirika hilo la Umoja wa Mataifa linaweza kujenga makaazi 6000 kwa familia za Wapalestina na linahusika kutoa misaada kwa waathiriwa wa vita waliopoteza makaazi yao.

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban ki Moon aliupigia debe mradi huo katika ziara yake katika eneo hilo siku ya jumapili alisema bado kuna mahitaji mengi kwa waathiriwa wengi wakiwa jamaa wa Wapalestina 1400 waliofariki katika mashambulio ya Israel.

Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu hata hivyo anasisitiza kwamba sera za serikali hazijabadilika na haoni ubaya wa ujenzi wa makaazi.

Netanyahu anatarajiwa kukutana na rais wa marekani Barack Obama hapo kesho kwa mazungumzo yanayotarajiwa kugusia mzozo huo wa ujenzi wa makaazi na ufufuzi wa mazungumzo ya amani na Wapalestina.

Mawaziri wa mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya katika mkutano wao mjini Brussels hii leo walijadili mbinu za kuipa Israel mbinyo dhidi ya kutojenga makaazi mashariki mwa Jerusalem kwa walowezi wa kiyahudi na pia walijadili mbinu za kufufua tena mazungumzo yatakoongozwa na pande nne zinazotafuta amani mashariki ya kati.

Mwandishi, Peter Moss/AFP/DPA

Mhariri, Abdul-Rahman