Umoja wa Afrika kupuuza waranti dhidi ya Gadaffi | Matukio ya Kisiasa | DW | 03.07.2011
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Umoja wa Afrika kupuuza waranti dhidi ya Gadaffi

Umoja wa Afrika umetoa mwito kwa nchi wanachama kupuuza waranti iliyotolewa na Mahakama ya Kimataifa ICC, dhidi ya Kiongozi wa Libya, Kanali Muammar Gaddafi.

default

Kiongozi wa Libya, Kanali Muammar Gaddafi

Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika, Jean Ping amesema, Mahakama ya Kimataifa mjini The Hague Uholanzi, inabagua. Mahakama hiyo inafuatiliza uhalifu uliotokea barani Afrika tu na hudharau uhalifu uliofanywa na nchi za Magharibi huko Iraq, Afghanistan au Pakistan.

Wakati huo huo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Hillary Clinton amemtaka kiongozi wa Libya Kanali Muammar Gadaffi kuondoka madarakani. Alitamka hayo, baada ya Gadaffi siku ya Ijumaa kuonya kuwa atashambulia miji ya Ulaya ili kulipiza kisasi operesheni ya NATO nchini Libya. Akiwa katika ziara rasmi nchini Uhispania, iliyo mshirika wa NATO, Clinton alisema, Gadaffi asaidie kuleta demokrasia badala ya kutoa vitisho.

 • Tarehe 03.07.2011
 • Mwandishi Martin,Prema/ZPR
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/RXH9
 • Tarehe 03.07.2011
 • Mwandishi Martin,Prema/ZPR
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/RXH9

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com