Ulimwengu wa michezo wataka majibu | Michezo | DW | 14.03.2016
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

Ulimwengu wa michezo wataka majibu

Wanamichezo na mamilioni ya mashabiki wa michezo kote duniani wanataka majibu kuhusiana na msururu wa kashfa za matumizi ya dawa za kuongeza misuli nguvu iliyoukumba ulimwengu wa michezo

Rais wa Shirika la Kimataifa la Kupambana na matumizi ya dawa za kuongeza misuli nguvu duniani – WADA Craig Reedie pia ametoa wito kwa wahisani kusaidia kufadhili vita dhidi ya dawa zilizopigwa marufuku michezoni na akaahidi kupewa ulinzi bora wanaofichua siri za uovu huo. "imani ya umma michezoni ilivunjwa kabisa katika mwaka wa 2015, hisia za umma zikaharibiwa, wasiwasi umetanda na kuna hisia ya jumla kuwa yote hayo yamekithiri. Tumeshuhudia maafisa wakuu wa FIFA wakikamatwa kwa tuhuma za uhalifu wa rushwa, matumizi ya zilizopigwa marufuku michezoni Urusi na mapungufu ya usimamizi unaohusiana na suala hilo katika IAAF. Tennis imetuhumiwa kuhusiana na upangaji mechi katika kiwango cha juu na wiki iliyopita mmoja wa nyota wake alikiri kutumia dawa za kuongeza misuli nguvu".

Wakati huo huo, WADA imeipa Kenya hadi Aprili 5 kuthibitisha kuwa inaweza kufanikiwa kulikabili suala la dawa zilizopigwa marufuku, au ifungiwe kushiriki katika michezo ya Olimpiki mjini Rio de Janiero Brazil.

Sebastian Coe ni rais wa Shirikisho la Kimataifa la Raidah – IAAF na hapa anazungumzia suala hilo huku akizitaja nchi ambazo zinafuatiliwa kwa makini "Kenya, Ukraine na Belarus zimewekwa kwenye orodha ya uchunguzi ya IAAF ya mwaka wa 2016 kuhakikisha kuwa mipango ya kitaifa ya kuapmbana na matumizi a dawa zilizopigwa marufuku michezoni inaimarishwa na hatua za kuitimiza mipango hiyo zinakamilishwa ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/AP/Reuters
Mhariri : Mohammed Abdul-Rahman

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com