Ulaya yakodowa macho Ujerumani na Italia jumapili inayokuja | Matukio ya Kisiasa | DW | 02.03.2018
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Ulaya yakodowa macho Ujerumani na Italia jumapili inayokuja

Wanachama wa SPD wamekamilisha zoezi la uchaguzi, kuamua juu ya mustakbali wa serikali ya muungano pamoja vyama vya CDU na CSU. Matokeo ya zoezi hilo yanasubiriwa kwa shauku kubwa ndani na nje ya mipaka ya Ujerumani

 

Marchi nne, au jumapili inayokuja mengi yatabainika kuhusu Ulaya: Italia wapiga kura kulichagua bunge jipya na Ujerumani itafahamika kama serikali ya muungano wa vyama vikuu au GroKo kati ya wahafidhina na wana Social Democrat itaendelea kutawala. Halmashauri kuu ya Umoja wa Ulaya inajiandaa pindi hali mbaya ikitokea" alisema hayo mwenyekiti wa halmashauri kuu ya Umoja wa ulaya Jean-Claude Juncker wiki iliyopita. Wasi wasi wake mkubwa unasababishwa na matokeo ya uchaguzi wa bunge nchini Italia: Ukosefu wa wingi madhubuti unaweza kuifanya nchi hiyo isitawalike.

Mkuu wa tawi la vijana wa SPD,mpinzani mkubwa wa makubaliano ya GroKo

Mkuu wa tawi la vijana wa SPD,mpinzani mkubwa wa makubaliano ya GroKo

Zoezi la uchaguzi miongoni mwa wanachama wa SPD linatia hofu

Jean Claude Juncker amelitaja pia zoezi la uchaguzi wa wanachama wa SPD kuwa ni sababu nyengine ya kuingiwa na hofu: Bila ya ridhaa ya wanachama wa SPD, itamaanisha serikali ya muungano wa vyama vikuu au Groko haitoundwa na kwa hivyo nchi inayoongoza barani Ulaya itakuwa haina serikali pia.

Kansela Angela Merkel anayatambua yote hayo. Katika hotuba yake ya  hivi karibuni bungeni kuhusu sera ya Ujerumani kuelekea Umoja wa ulaya, kansela Merkel alisema "wanahitaji mapambazuko barani Ulaya."Na hivyo ndivyo ilivyotajwa katika mkataba ya kuunda serikali ya muungano kati ya wahafidhina na wana Social Democrat, uliochapishwa mapema mwezi uliopita. "Mwaka 2018 ni mwaka unaobidi kufungua  njia za mageuzi" alisema katika hotuba yake bungeni.

Wataalam hawaoni kishindo kikubwa kutokea

Ndo kusema zahma itapiga mjini Brusels ikiwa serikali ya muungano wa vyama vikuu haitoweza kuundwa mjini Berlin? Janis Emmanouillidis wa kituo cha sera za Ulaya mjini Brussels anasema anasemay "Haamini kama kutatokea patashika. Bila ya shaka hali hiyo haitowafanya watu wapumuwe. Watu wanaamini serikali ya muungano wa vyama vikuu itaundwa. Kama haitokuwepo basi itamaanisha, aina fulani ya wasi wasi utatanda barani Ulaya kwasababu mmojawapo wa wadau muhimu angekuwa hana serikali ambayo itakuwa na uwezo wa kudhamini maamuzi muhimu."

Lakini hata kama serikali ya muungano itaundwa, Angela Merkel hatoangaliwa  tena kama "kiongozi asiyebishika barani Ulaya" kama alivyokuwa kabla ya uchaguzi mkuu wa September 2017. Jarida la Marekani Times linamtaja rais wa Ufaransa Emmanuel Macron "kuwa mshika bendera mpya wa ulaya. Katika wakati ambapo chama cha kansela Merkel CDU kilipoteza zaidi ya asili mia 7 katika uchaguzi mkuu uliopita, Macron aliibuka na ushindi mkubwa katika uchagizi wa rais mwaka huo huo wa 2017 nchini Ufaransa.

Kansela Angela Merkel

Kansela Angela Merkel

Macron anyemelea nafasi ya Merkel kama mshika bendera barani Ulaya

Katika wakati ambapo Macron anawakaribisha mjini Paris viongozi washupavu mfano wa Donald Trump, Putin na Erdogan, Merkel amekuwa kwa miezi  sasa akijaribu kujadiliana na viongozi wa vyama vya kisiasa ili kuunda serikali ya muungano.

Macron hawezi kumifikia daraja ya Merkel anasema Stefan Seidendorf, ambae ni naibu mwenyekiti wa taasisi ya uhusiano kati ya Ujerumani na Ufaransa mjini Ludwigsburg. Anahoji hata hivyo Macron anayatumia kikamilifu madaraka ya jamhuri ya tano, naiwe kidiplomasia au kijeshi ili kuimarisha ushawishi wa Ufaransa barani Ulaya na ulimwenguni kwa jumla.

 

Mwandishi: Hasselbach,Christoph/ Hamidou Oummilkheir

Mhariri:Josephat Charo

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com