1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ulaya, China, Urusi kujadili makubaliano mapya na Iran

Sekione Kitojo
20 Mei 2018

Wanadiplomasia kutoka Ulaya, China na Urusi wanajadili mkataba mpya kuipatia Iran msaada wa fedha kuzuwia utengenezaji wa makombora na uingiliaj kati katika kanda ya mashariki ya kati.

https://p.dw.com/p/2y1MJ
Iran Atomgespräche 18.03.2014
Picha: Dieter Nagl/AFP/Getty Images

Mazungumzo  hayo yana  matumaini  ya  kuokoa  makubaliano  ya kinyuklia ya mwaka 2015, limesema gazeti  la  Ujeruamni leo Jumapili(20.05.2018).

Belgien Brussel - Irans Außenminister Javad Zarif und Federica Mogherini
Waziri wa mambo ya kigeni wa Iran javad Zarif (kushoto) akizungumza na mkuu wa sera za mambo ya kigeni wa EU Federica MogheriniPicha: Reuters/T. Monasse

Maafisa  watakutana  mjini  Vienna katika  wiki  zijazo chini  ya uongozi wa  mwanadiplomasia  mwandamizi wa Umoja  wa  Ulaya Helga Schmid kujadili hatua  inayofuata  baada  ya  uamuzi  wa  Mei 8 wa rais  wa  Marekani  Donald  Trump kujitoa  kutoka  katika makubaliano  ya  mwaka  2015 na Iran, gazeti  la  kila  Jumapili  la Welt am Sontag limeandika , likinukuu vyanzo za maafisa waandamizi wa  Umoja  wa  Ulaya.

Ujerumani, Ufaransa, Uingereza, Urusi na  China zitashiriki katika mkutano  huo, lakini Marekani  haitashiriki, limesema gazeti  hilo. Haikufahamika  mara  moja  iwapo  Iran, ambayo  imekuwa  ikikataa miito  ya  kuzuwia  mpango  wake  wa  makombora hapo  kabla , iwapo  itashiriki.

Chini  ya  makubaliano  ya  mwaka  2015, Iran ilikubali  kuzuwia mpango  wake  wa  kinyuklia  ili  kuweza  kuondolewa  vikwazo vingi vya  mataifa  ya  magharibi.

Moja  kati  ya  malalamiko  makubwa  ya  utawala  wa  Trump ilikuwa kwamba  mkataba  huo  haukuhusisha  mpango  wa  makombora  wa Iran ama  uungwaji  wake  mkono  makundi  yenye  silaha   katika mashariki  ya  kati ambayo  mataifa  ya  magharibi  yanayaona kuwa  ni  magaidi.

Belgien EU-Außenministertreffen
Mawaziri wa mambo ya kigeni wa mataifa ya Ufaransa, Ujerumani , Uingereza na Umoja wa ulaya wakiwa na waziri wa mambo ya kigeni wa Iran javad Zarif (wa pili kutoka kushoto)Picha: picture-alliance/Photoshot

Kumshawishi Trump kufuta  vikwazo dhidi ya  Iran

Kukamilisha  makubaliano  mapya  ambayo  yataendeleza  vifungu vya kinyuklia na  kuzuwia  juhudi  za  kuendeleza  utengenezaji  wa makombora  pamoja  na  shughuli  za  Iran  katika  kanda  hiyo kunaweza  kumshawishi  Trump  kuondoa  vikwazo  dhidi  ya  Iran , gazeti  hilo  limesema.

"Tunapaswa  kujiondoa  kutoka  katika  jina  la  "makubaliano ya kinyuklia  ya Vienna" na  kuongeza  vitu  vichache  vya  ziada. Ni hivyo  tu  ambapo  vitamshawishi rais  Trump  kukubali  na  kuondoa vikwazo tena," gazeti  hilo  limemnukuu mwanadiplomasia mwandamizi  wa  Umoja  wa  Ulaya  akisema.

 

Hakuna maelezo  ya  haraka  yaliyopatikana  kutoka  katika  wizara ya  mambo  ya  kigeni  ya  Ujerumani.

Mkuu  wa  masuala  ya  nishati  wa  Umoja  wa  Ulaya  alitaka kuihakikishia  Iran   Jumamosi  kwamba  kundi  la  mataifa  28  ya Umoja  huo  yanaendelea kuwa  na  dhamira  ya  kuyaokoa makubaliano  ya  kinyuklia, na  kuimarisha  biashara  na  Iran.

Maafisa  kutoka  Umoja  wa  Ulaya, Ujerumani  na  mataifa  mengine ambayo  yamebakia  katika  makubaliani  wamesema  itakuwa maafa  iwapo juhudi  za EU  zitashindwa  kuyalinda  makubaliano hayo.

China Mohammed Dschawad Sarif, Außenminister Iran mit Wang Yi, Außenminister
Waziri wa mambo ya kigeni wa Iran Javad zarif(kushoto) akikutana na waziri mwenzake wa China wang YiPicha: Reuters/T. Peter

Wawekezaji  wameshindwa  kuwekeza  Iran

Iran imehangaika  kufanikisha  manufaa ya  kifedha  kutokana  na makubaliano  hayo, kwa  sababu  kwa  sehemu  vikwazo  vilivyobaki vya  Marekani  kuhusiana  na  mpango  wake  wa  makombora vimezuwia  wawekezaji  wakuu  wa  mataifa  ya  magharibi  kufanya biashara na  Iran.

Maafisa  wanatafuta  njia  mpya  kutokana  na  kufahamu  kwamba itakuwa  vigumu  kwa  makampuni  ya  Ulaya  kuepuka  vikwazo vipya  vya  Marekani, gazeti  hilo  limeripoti.

Kasachstan Syriengespräche in Astana
Waziri Javad Zarif wa Iran (kulia) pamoja na waziri mwenzake wa Urusi Sergei Lavrov(katikati)Picha: Reuters/M. Kholdorbekov

Gazeti  hilo  limesema  makubaliano  mapya  yanaweza  kujumuisha mabilioni  ya  dola  ya  msaada  wa  kifedha   kwa  Iran, sambamba na makubaliano  ya  Umoja  wa  Ulaya   ambayo  yanatoa  mabilioni kama  msaada  kwa  Uturuki kwa  kuwachukua  mamilioni  ya wahamiaji  na  kufunga  mipaka  yake, hatua  iliyosaidia  kufikisha mwisho mzozo  wa  wahamiaji.

Iran  na  mataifa  makubwa  ya  Ulaya  zimeanza  vizuri  mazungumzo kuhusiana  na  jinsi  ya  kuokoa  makubaliano  hayo  ya  mwaka 2015  lakini  itategemea  juu  ya  nini  kitatokea  katika  wiki  chache zijazo, waziri  wa  mambo  ya  kigeni  wa  Iran Mohammed javad zarif amesema  wiki  iliyopita.

Mwandishi: Sekione Kitojo / rtre

Mhariri: Daniel Gakuba