1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroUkraine

Ukraine yasema mashambulizi yanahatarisha ugavi wa umeme

Amina Mjahid
29 Machi 2024

Serikali ya Ukraine imeonya kuwa mashambulizi ya angani ya Urusi yanaweka hatarini ugavi wa nishati ya umeme.

https://p.dw.com/p/4eG8x
Bwawa la umeme la Dniester nchini Ukraine
Bwawa la umeme la Dniester nchini UkrainePicha: Adam Chuck/IMAGO/YAY Images

Mashambulizi hayo yamesababisha mauaji ya mwanamume mmoja wa miaka 39 na kumjeruhi mtu mwingine mmoja katika shambulizi lililotokea Kusini Mashariki mwa mji wa Nikopol huku mashambulizi mengine ya angani katika eneo la Kamianske yakiwajeruhi watu watano akiwemo mtoto.

Katika wiki za hivi karibuni Urusi imeendeleza mashambulizi yake Kiev yakilenga miundo mbinu ikijibu mashambulizi ya Ukraine katika maeneo ya mpakani ya Urusi. Ukraine imeendelea kuwasisitizia washirika wake wa Magharibi kwamba inahitaji mifumo zaidi ya kujilinda na makombora ili kupambana na uvamizi wa Urusi nchini mwake.