Ukraine yarusha zaidi ya droni 280 kulekea Urusi
21 Machi 2026
Matangazo
Katika chapisho kwenye mtandao wa Telegram, Gavana wa eneo la kusini la Rostov Yuri Slyusar, amesema takriban droni 90 zilidunguliwa katika eneo hilo.
Kwa upande wake, meya wa Moscow Sergei Sobyanin, ameripoti kuwa droni 27 zilizoelekezwa katika mji huo mkuu pia zilidunguliwa.
Gavana wa eneo la kusini magharibi la Saratov Roman Busargin, pia ameripoti kuuawa kwa watu wawili katika mashambulizi ya droni yalioharibu nyumba kadhaa.
Kulingana na wizara hiyo ya ulinzi, jumla ya droni 283 zimedunguliwa.
Katika kulipiza kisasi cha mashambulizi ya Urusi ambayo yamelenga eneo lake kila siku tangu mwaka 2022, Ukraine imekuwa ikishambulia mara kwa mara ndani ya Urusi, ikisema kimsingi inalenga miundombinu ya nishati na ya kijeshi.