1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani yathibitisha mgonjwa wa kwanza wa Corona

Lilian Mtono
28 Januari 2020

Mgonjwa wa kwanza wa maradhi yanayosababishwa na virusi vya Corona amethibitishwa nchini Ujerumani.

https://p.dw.com/p/3Wtk5
Coronavirus
Picha: imago/Science Photo Library

Mgonjwa wa kwanza wa maradhi yanayosababishwa na virusi vya Corona amethibitishwa nchini Ujerumani. Msemaji wa wizara ya afya mjini Munich, amesema jana jioni kwamba mgonjwa huyo ni mwanaume anayetokea eneo la Stanberg, katika jimbo la Bavaria, kiasi kilomita 30 kusini magharibi mwa Munich.

Jamaa wa karibu na mgonjwa huyo wameelezewa kuhusu dalili za maradhi hayo, hatua za usafi na namna virusi hivyo vinavyosambaa.

Kirusi hicho kipya aina ya Corona kimetokea katika mji wa Wuhan nchini China hadi sasa kimesababisha vifo vya takriban watu 106. Tume ya afya katika jimbo la Hubei ambako ni kitovu vya maradhi hayo imesema watu wengine 24 wamekufa na 1,291 wameambukizwa, idadi inayofanya jumla ya watu walioambukizwa hadi sasa kufikia 4,000 kote nchini humo.

Visa vingine vya Corona vimeripotiwa Korea Kusini, Taiwan, Thailand, Nepal, Vietnam, Saudi Arabia, Singapore, Marekani, Ufaransa na Australia.