1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani yasherehekea miaka 20 ya kuungana

3 Oktoba 2010

Wajerumani wanakumbuka miaka 20 tangu walipoungana baada ya kutengena kwa miongo minne.

https://p.dw.com/p/PTCd
Ukuta wa Berlin uliigawanya Ujerumani kwa miongo minne.Picha: AP

BERLIN

Sherehe  zimeanza  nchini  Ujerumani  kuadhimisha  miaka  20  tangu  pale  Ujerumani Magharibi na Mashariki zilipoungana,  ambapo  kutakuwa  na  sherehe  katika  mitaa mbali  mbali  pamoja  na  matamasha  ya  muziki  katika  mji  mkuu  Berlin,   Bremen na  kwingineko. Tarehe  3  Oktoba , 1990  Ujerumani  iliungana  baada  ya  kutengana kwa miongo  minne . Ukuta  wa  Berlin  ulianguka  kiasi  miezi  11  kabla  wakati Wajerumani  waliposherehekea  muungano  wao  mbele  ya   bunge  mjini  Berlin. Tangu wakati huo, Oktoba 3  ni  siku  ya  mapumziko . Mwaka  huu  mji  wa Bremen ndio umepewa hadhi ya kuanda rasmi  sherehe  hizo. Maafisa  wa  mji  huo walitengeneza mfano wa Ukuta wa Berlin, kama kumbukumbu ya historia ya ukuta huo ulivyotenganisha Ujerumani mbili. Kansela  Angela  Merkel anasubiriwa kutoa hotuba baadaye leo mjini Bremen.