Ujerumani yamkubali mrithi wa Putin | Habari za Ulimwengu | DW | 11.12.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Ujerumani yamkubali mrithi wa Putin

BERLIN.Ujerumani imeupokea uamuzi wa Rais Vladmir Putin wa Urusi kumuidhinisha Makamu wa kwanza wa Waziri Mkuu Dmitry Medvedev kuwa mrithi wake wakati atakapog´atuka mwezi March mwakani.

Waziri wa nchi katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Ujerumani Gernot Erler amesema kuwa Medvedev huenda akawa na mtizimo tofauti na uongozi wa sasa wa Urusi.

Amesema kuwa Ujerumani inatiwa tamaa na Medvedev kutokana na kwamba hana historia ya kuwa jasusi au mwanajeshi hapo kabla.

Wafuatiliaji wa siasa za Urusi wanasema kuwa Medvedev mwenye umri wa miaka 42 na ambaye kitaaluma ni mwanasheria, ana nafasi kubwa ya kushinda.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com