1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani yalipiza kisasi dhidi ya Uholanzi

Bruce Amani
25 Machi 2019

Timu mpya ya Ujerumani ilionyesha kwa kiasi umahiri wake wa siku za nyuma kutokana na aina ya mchezo lakini pia ilihitaji kiasi fulani cha bahati katika ushindi wa 3 – 2 dhidi ya mahasimu wao wakali Uholanzi

https://p.dw.com/p/3Fd1x
Euro 2020 Qualifikation Niederlande Deutschland Jubel
Picha: Reuters/P. van de Wouw

Timu mpya ya Ujerumani ilionyesha kwa kiasi umahiri wake wa siku za nyuma kutokana na aina ya mchezo lakini pia ilihitaji kiasi fulani cha bahati katika ushindi wa 3 – 2 dhidi ya mahasimu wao wakali Uholanzi na kuweka mwanzo mzuri katika kampeni ya kutinga mashindano ya Euro 2020.

Ujerumani ilifunga bao la tatu kutokana na shambulizi la kasi kuanzia nyuma kabla ya Nico Schulz kuweka mpira kambani katika dakika ya 90.

Mchezo huo ulirejesha kumbukumbu za kiwango ambacho timu ya Loew ilikuwa nacho kwa mwongo mzima na kushinda Kombe la Dunia 2014 kabla ya kusambaratika mwaka jana, kwa kubanduliwa nje ya Kombe la Dunia hatua ya makundi na kushushwa kutoka michuano ya daraja la A la Ligi ya Mataifa.

Na hayo yalifanyika katika uwanja wa Amsterdam Arena ambako Ujerumani walizabwa 3 – 0 Oktoba mwaka jana na kumuonyesha Loew umuhimu wa kukifanyia kikosi chake mabaliko makubwa. Kiungo Toni Kroos na kipa Manuel Neuer ndio waliosalia tu kutoka kwenye kikosi cha fainali ya 2014. Mabao mengine ya Ujerumani jana yalifungwa na Leroy Sane na Serge Gnabry. Kabla ya mechi ya jana, Ujerumani ilitoka sare ya 1 – 1 na Serbia katika mchuano wa kirafiki.