Ujerumani yakiri kupokea taarifa za uwezekano wa kushambuliwa na magaidi | Habari za Ulimwengu | DW | 13.01.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Ujerumani yakiri kupokea taarifa za uwezekano wa kushambuliwa na magaidi

BERLIN:

SERIKALI YA Ujerumani inasema imepokea onyo kutoka kwa wakuu wa Lebanon kuwa watu wenye imani kali wanapanga kufanya shambulizi la kigaidi nchini Ujerumani.

Maafisa wanasema wamepewa tahadhari hiyo baada ya maafisa wa Lebanon kumkamata mtu mmoja anaeshukiwa ni mshirika wa kundi la kigaidi la al-Qaida mjini Beirut.Mtuhumiwa huyo anaaminika kuwa ameupigia simu ubalozi wa Ujerumani mjini Beirut mapema wiki hii.akidaiwa kuwa ametishia kufanya shambulizi katika maeneo ya kiusalama ya Ujeruamni kwa kulipiza kisasi kwa ajili ya kuhukumiwa mtuhumiwa wa kundi la al-Qaida nchini Ujerumani.

Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com