1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani yaizingatia India kama mshirika muhimu

5 Desemba 2022

Waziri wa mambo ya kigeni wa Ujerumani Annalena Baerbock aliye ziarani nchini India amesema leo serikali mjini Berlin inaizingatia India kuwa mshirika muhimu katika masuala ya uchumi na usalama.

https://p.dw.com/p/4KUkz
Indien Neu Delhi | Außenministerin Baerbock und Außenminister Subrahmanyam Jaishankar
Picha: Minister S. Jaishankar's Twitter handle/AP/picture alliance

Waziri Baerbock, akizungumza katika mkutano na waandishi habari mjini New Delhi baada ya mazungumzo na mwenzake wa India Subrahmanyam Jaishankar, Bibi Baerbock amesema serikali ya Ujerumani inataka kutanua zaidi mahusiano yake na India.

Akijibu swali juu ya iwapo India itachukua nafasi ya ushirikiano uliopo kati ya Ujerumani na China bibi Baerbock amesema, "Hapana, ndiyo jibu fupi kwa swali hilo la kubadilisha mshirika, kwa sababu wakati wote India imekuwa mshirika wa Ujerumani na Umoja wa Ulaya lakini tunataka kuongeza zaidi ushirika huu"

Mapema hii leo Baerbock na mwenzake wa India walishuhudia utiaji saini wa makubaliano yatakayowezesha wanafunzi na raia wa India wenye ujuzi kuingia Ujerumani bila vizingiti.

Ujerumani na India zimeashiria kuwa tayari kupanua ushirikiano katika masuala ya kiuchumi na mazingira baada ya mkutano wa leo kati ya mawaziri wa mambo ya nje wa mataifa hayo mawili.