1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani yagombea kiti katika Baraza la Usalama

21 Septemba 2010

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Guido Westerwelle ameelekea New York kuhudhuria mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

https://p.dw.com/p/PIRx
Aussenminister Guido Westerwelle (FDP), spricht am Mittwoch (15.09.10) im Bundestag in Berlin. Mit der traditionellen Generaldebatte setzt der Bundestag am Mittwoch seine viertaegigen Haushaltsberatungen fort. Foto: Maya Hitij/dapd
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Guido Westerwelle.Picha: AP

Mbali na kuhotubia baraza hilo jumamosi ijayo, waziri huyo wa nje ataipigia debe Ujerumani kuchaguliwa mwanachama asie wa kudumu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa linapokutana kila mwaka katika mwezi wa Septemba mjini New York, wajumbe kutoka nchi wanachama 192 hukusanyika katika makao makuu ya umoja huo. Kila nchi mwanachama hupata nafasi ya kulihotubia baraza hilo. Hiyo ni heshima maalum, kwani hotuba hiyo husikilizwa kila pembe ya dunia.

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ni jukwaa la kuwasiliana; ni soko la diplomasia. Na mada mojawapo muhimu ya Westerwelle inahusika na udhibiti wa silaha kote duniani. Amesema:

"Pamoja na Japan na Australia, Ujerumani itakuwa mmojawapo wa waasisi katika kundi la nchi zitakazojitahidi kupata maendeleo katika suala la kudhibiti silaha na kuzuia uenezaji wa silaha za kinyuklia. "

Mada nyingine itakayogusiwa na waziri wa nje wa Ujerumani wakati wa majadiliano yake mjini New York ni ombi la Ujerumani kuchaguliwa mwanachama asiedumu katika Baraza la Usalama. Tarehe 12 Oktoba, mabalozi 192 katika Umoja wa Mataifa wataamua iwapo kuanzia mwaka 2011, Ujerumani itakuwa mwanachama katika Baraza la Usalama kwa kipindi cha miaka miwili. Hilo ni baraza muhimu kabisa kuhusu sera za usalama duniani.

Angela Merkel, Chancellor of Germany, addresses a summit on the Millennium Development Goals at United Nations headquarters on Tuesday, Sept. 21, 2010. (AP Photo/Richard Drew)
Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel akihotubia mkutano wa kilele wa Malengo ya Maendeleo ya Milenia , Septemba 21, 2010, mjini New York.Picha: AP

Kwa upande mwingine, malengo ya maendeleo ya milenia ni mada itakayopewa kipaumbele na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel, atakapohotubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa baadae leo hii. Kwa maoni yake malengo yaliyokubaliwa miaka kumi iliyopita yanapaswa kutimizwa ifikapo mwaka 2015. Lakini hata nchi zinazopokea misaada zinapaswa kuwajibika zaidi katika jitahada za kupunguza umasikini, vifo vya watoto wadogo na akina mama pamoja na kupiga vita magonjwa ya maambukizo. Merkel anasema kuwa nchi hizo zipatiwe msaada ikiwa tu imeonekana kuwa maendeleo yamepatikana kuelekea malengo hayo ya milenia.

Wakati huo huo, viongozi wa Umoja wa Ulaya wanaoshiriki katika mkutano wa Malengo ya Maendeleo ya Milenia mjini New York, wameahidi msaada wa Euro bilioni moja kupiga vita umasikini duniani.

U.N. Secretary-General Ban Ki-moon addresses a summit on the Millennium Development Goals at United Nations headquarters on Monday, Sept. 20, 2010. (AP Photo/Richard Drew)
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon akihotubia mkutano wa kilele wa Malengo ya Maendeleo ya Milenia,Septemba 20, 2010 katika makao makuu ya umoja huo mjini New York.Picha: AP

Hapo awali Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban ki-Moon alisema bado inawezekana kutimiza malengo manane makuu ya maendeleo ifikapo mwaka 2015, ikiwa kutakuwepo nia ya kisiasa na viongozi wa kimataifa watatoa fedha zinazohitajika.

Mwandishi: Werkhäuser,Nina/ZPR

Mpitiaji: M.Abdul-Rahman