Ujerumani yafunga ubalozi wake wa Moscow, Urusi | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 07.08.2010
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Timu Yetu

Ujerumani yafunga ubalozi wake wa Moscow, Urusi

Ubalozi huo umefungwa kutokana na moshi uliosababishwa na moto unaoendelea kuwaka nchini humo.

Moto ukiwaka katika misitu nchini Urusi.

Moto ukiwaka katika misitu nchini Urusi.

Mji mkuu wa Urusi, Moscow, unakabiliwa na moshi kutokana na moto mkubwa ambao umekuwa ukiwaka katika maeneo mbalimbali nchini humo tangu wiki iliyopita. Ndege zilizokuwa zikielekea mjini humo zimeelekezwa kutua katika viwanja vingine vya ndege kutokana na moshi huo.

Uchafuzi wa hewa mjini Moscow umeongezeka mara tano kuliko viwango vya kawaida. Ujerumani imeufunga ubalozi wake mjini Moscow kutokana na moshi huo na kuwaonya raia wake, hususan wenye matatizo ya kupumua na watoto wasiende katika maeneo yaliyoathiriwa.

Moto nchini Urusi unaendelea kuwaka kutokana na upepo mkali na kiwango kikubwa cha joto cha zaidi ya nyuzi za joto 40 katika kipimo cha Celcius. Watu 52 wamekufa nchini Urusi kutokana na moto huo ambao pia unawaka katika nchi jirani ya Ukraine. Serikali imelituma jeshi kuifunga misitu na kuyalinda maeneo ya kuhifadhia silaha.

 • Tarehe 07.08.2010
 • Mwandishi Kabogo Grace Patricia
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/OeO6
 • Tarehe 07.08.2010
 • Mwandishi Kabogo Grace Patricia
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/OeO6
Matangazo

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com