1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani yachunguza ripoti kuhusu kutekwa nyara raia wake mwengine wa kike nchini Afghanistan

18 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBXx

Berlin/Kabul:

Wizara ya mambo ya nchi za nje ya Ujerumani inasema inachunguza ripoti za kutekwa nyara bibvi mmoja wa kijerumani nchini Afghanistan.Kwa mujibu wa wizara ya mambo ya ndani ya Afghanistan mjini Kabul,mtumishi mmoja wa kike wa shirika la misaada la kikristo ametekwa nyara alipokua mkahawani maagharibi ya mji mkuu Kabul.Wizara ya mambo ya ndani ya Afghanistan imesema,wateka nyara wamefanikiwa kutoroka licha ya kuandamwa wakati huo huo na polisi.Hatima ya mhandisi wa kijerumani aliyetekwa nyara hivi karibuni nayo pia haijulikani,licha ya juhudi za kutaka aachiliwe huru.