Ujerumani yaadhimisha Siku ya Muungano | Matukio ya Kisiasa | DW | 03.10.2011
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Matukio ya Kisiasa

Ujerumani yaadhimisha Siku ya Muungano

Leo Ujerumani inaadhimisha miaka 21 ya kuungana upya baada ya kugawika kwa miaka arobaini wakati wa vita baridi.

German Chancellor Angela Merkel reacts during the debate about the eurozone bailout fund at the German parliament Bundestag in Berlin, Germany, Thursday, Sept. 29, 2011. German lawmakers are expected to approve new powers Thursday for the eurozone bailout fund in a major step toward tackling the bloc's sprawling sovereign debt crisis. (Foto:Markus Schreiber/AP/dapd)

Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel asema, kuna mengi ya kujivunia muungano upya

Kansela Angela Merkel na Rais Christian Wulff wa Ujerumani ni miongoni mwa viongozi mashahuri wanaohudhuria sherehe kuu za kuadhimisha muungano wa Ujerumani aambazo mwaka huu zinafanywa katika mji mkuu wa zamani wa Ujerumani ya Magharibi, Bonn. Sherehe za muungano wa Ujerumani zimefunguliwa rasmi leo hii katika mji wa Bonn kwa misa ya ekumeni iliyohudhuriwa na takribana wageni elfu moja chini ya ulinzi mkali. Miongoni mwa wageni mashuhuri ni Kansela Angela Merkel, Rais Christian Wulff, Rais wa Bunge la Ujerumani Norbert Lammert.

Besucher des NRW-Tages gehen am Sonntag (02.10.11) in Bonn waehrend des Deutschlandfestes im Hofgarten der Universitaet Bonn zwischen den Staenden entlang. Mit einem grossen Deutschlandfest feiert Nordrhein-Westfalen bis Montag (03.10.11) in Bonn seinen 65. Landesgeburtstag und zugleich den Tag der Deutschen Einheit. (zu dapd-Text) Foto: Timur Emek/dapd

Rais wa Ujerumani, Christian Wulff (kulia) akijumuika na wananchi kwenye sherehe za NRW, Bonn

Baadae sherehe za muungano wa Ujerumani zitaendelea katika bunge la zamani la mjini Bonn ambako Rais wa Baraza la serikali za mikoa-Bundesrat, Hannelore Kraft alie pia waziri mkuu wa jimbo la North-Rhine Westphalia-(NRW) na Rais wa Mahakama ya Katiba ya Ujerumani, Andreas Voßkuhle watatoa hotuba kuu. Sherehe za miaka 21 ya muungano wa Ujerumani zinafanywa pamoja na sherehe za kuadhimisha miaka 65 ya kuundwa jimbo la North-Rhine Westfalia na zimeanza tangu siku ya jumamosi. Mamia ya watu wanasongana katika maeneo maalum yaliyotengwa kwa sherehe hizo ambako majimbo 16 ya Ujerumani yanawakilishwa sawa na idara mbali mbali za serikali ya jimbo la Northrhine Westphalia na mji wa Bonn.

Deutsche Welle pia kama sehemu ya sherehe za muungano wa Ujerumani hapo jana, ilikuwa na tafrija maalum ambapo kwa mara ya kumi imetoa "Zawadi ya Muungano". Mshindi hutunukiwa zawadi hiyo kama kitambulisho cha mchango na jitahada zake za kuzileta karibu zaidi pande mbili za Ujerumani. Tangu mwezi wa Septemba watu binafsi na mashirika yameshindana kuchaguliwa na jopo huru la majaji chini ya uenyekiti wa Joachim Gauck. Washindi hao wamechaguliwa chini ya kundi la vijana, utamaduni na binadamu. Kutoka kila kundi, wamepatikana washindi wawili na wamegawana zawadi hiyo ya muungano iliyo na thamani ya Euro 15,000.

Die Vorsitzende der SPD in Nordrhein-Westfalen, Hannelore Kraft, spricht am Samstag,10. Juli 2010, in Koeln beim ausserordentlichen Landesparteitag der nordrhein-westfaelischen SPD zu den Delegierten. In Nordrhein-Westfalen entscheidet am Samstag die Parteibasis von SPD und Gruenen ueber die geplante rot-gruene Minderheitsregierung. (apn Photo/Roberto Pfeil) --- ---North Rhine Westphalia's Social Democratic party chairwoman Hannelore Kraft speaks to the deleagtes of a special party convent in Cologne, Germany, Saturday, July 10, 2010. The delegates will discuss the coaltions contract withe the Greens. (apn Photo/Roberto Pfeil)

Waziri Mkuu wa jimbo la North-Rhine Westphalia, Hannelore Kraft

Kabla ya sherehe za leo kufunguliwa rasmi, Kansela Merkel aliekulia Ujerumani ya Mashariki alisema, bado kuna tofauti kubwa na hasa katika soko la ajira ambapo ukosefu wa ajira ni mkubwa zaidi upande wa mashariki. Katika hotuba yake ya kila wiki kwenye mtandao, Merkel amesema hata hivyo kuna mengi ya kufuarhia muungano huo upya. Ujerumani ya Magharibi na Ujerumani ya Mashariki ya kikomunisti ziliungana tarehe 3 Oktoba mwaka 1990, yaani chini ya miezi 11 baada ya Ukuta wa Berlin kufunguliwa.

Mwandishi: Martin,Prema

Mhariri:Othman, Miraji

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com