1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani, Ubelgiji, Marekani na Algeria zatinga awamu ya mchujo

Admin.WagnerD27 Juni 2014

Ujerumani imeingia duru ya mtoano kwa kuichapa Marekani 1-0. Bao hilo la pekee lilitiwa wavuni na mshambuliaji matata wa Ujerumani Thomas Müller katika dakika ya 55 baada ya kona iliyopigwa na Mesut Ozil

https://p.dw.com/p/1CRIJ
FIFA Fußball WM 2014 Deutschland USA
Picha: Getty Images

Kipa wa Marekani Tim Howard alifaulu kuutoa mpira uliopigwa kwa kichwa na Per Martesacker wa Ujerumani lakini mpira huo ukamuendea Mueller ambaye alivurumishwa mkwaju ulioutikisa wavu wa Marekani. Akizungumza baada ya mechi hiyo kumalizika Mueller amesema.. "Cha muhimu ni kwamba tumefunga bao moja na wapinzani wetu hawakupata kitu. Nadhani sisi tulikuwa timu iliyodhibiti mchezo na tulicheza vizuri sana katika kipindi cha kwanza, hususan mwanzoni mwa mchauno. Mara mbili au tatu tulikaribia kufung alakini haikuw arahisi kwani Wamarekani walikuwa wakirudi nyumba kulinda lango lao, kwa hiyo kawaida unakuwa mchezo wa kuvumilia. Kwa ujumla tumecheza ngoma kisawasawa dhidi ya timu kali ya Marekani kwa zaidi ya dakika 90. Tumeshinda bao moja kwa bila tu, lakini naukubali ushindi huo."

Thomas Mueller, ambaya sasa ana jumla ya magoli manne pamoja na Neymar wa Brazil na Lionel Messi wa Argentina, alicheza licha ya kushonwa mara tano katika sehemu ya juu ya jicho lake la kulia kufuatia jeraha alilopata wakati Ujerumani ilipocheza dhidi ya Ghana na kutoka sare ya mabao mawili kwa mawili Jumamosi iliyopita.

FIFA Fußball WM 2014 USA Deutschland
Kocha wa Ujerumani Joachim LöwPicha: Reuters

Baada ya mtanange kumalizika kocha wa Ujerumani Joachim Loew alisalimiana na kocha wa Marekani, Jurgen Klinsman, bosi wake wa zamani, wote wakitabasamu kwa kuwa timu zao zinasonga mbele, Ujerumani ikiwa kileleni mwa kundi G ikifuatiwa na Marekani katika nafasi ya pili. Loew amesema:

"Tumeudhibiti mchezo. Tumeshinda kwa kuwa tulistahiki. Tumecheza vizuri, tumecheza kwa umakini na tumejaribu kushambulia. Kitu ambacho tunaweza kukiboresha ni kutafuta njia za kutumia fursa zetu vizuri zaidi, na kuwa na uhakika mpira unakwenda kwa nani wakati wa pasi ya mwisho. Kama tungefanya hivyo leo tungefunga magoli matatu au zaidi."

Trainer Jürgen Klinsmann
Mkufunzi wa Marekani Jürgen KlinsmannPicha: picture-alliance/ZB

Hata kama Marekani ingetoka sare na Ujerumani timu zote mbili zingesonga mbele. Ujerumani sasa inakwenda Porto Alegre kucheza na Algeria, iliyomaliza ya pili katika kundi H nyuma ya Ubelgiji, ambayo itachuana na Marekani. Ubelgiji iliishinda Korea Kusini bao moja kwa bila na Algeria ikatoka sare ya bao moja kwa moja na Urusi katika mechi zilizochezwa pia jana. Hii ni mara ya kwanza kwa Algeria kufuzu kwa raundi ya pili ya timu 16 bora.

Rais wa Marekani Barack Obama ameliongoza taifa katika kusherehekea kufuzu kwa timu yao kwa duru ya pili ya mtoano. "Nalazimika kuanza kwa kuipongeza timu yetu ya soka kwa kusong ambele kwa raudi ya mtoano katika mashindano yakombe la dunia. Tulikuw akatika kundi lililojulikana kama kundi la kifo na ingawa hakutushinda leo, tumefuzu. Kwa hiyo tungali na fursa yya kushinda kombe la dunia na tunajivunia vijana wetu."

Mashabiki wa Marekani nao hawakuwachwa nyuma kama Djanira Schaefer: "Ulikuwa mchezo wa kusisimua. Ushindi wa bao moja kwa bila kwa Ujerumani lakini na sisi tumesonga mbele. Na tutasonga mbele hadi tufike fainali na bila shaka tutafaulu."

Katika mechi nyingine ya kundi G, Ghana imetolewa saa chache baada ya Sulley Muntari na Kevin-Prince Boateng kufukuzwa kwenye kikosi kwa kukosana na uongozi wa timu. Hatima ya Ghana iliamuliwa wakati Ureno ilipoizaba mabao 2-1.

Mwandishi: Josephat Charo/AFPE/APE
Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman