Ujerumani tayari kupambana na Georgia | Michezo | DW | 27.03.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Michezo

Ujerumani tayari kupambana na Georgia

Mshambuliaji wa Ujerumani Karim Bellarabi na beki Holger Badstuber wataukosa mchuano wa kufuzu katika dimba la mataifa ya Ulaya – Euro 2016 dhidi ya Georgia.

Naibu kocha wa Ujerumani Thomas Schneider amesema Bellarabi anaugua mafua wakati Badstuber akipatwa na maumivu ya misuli baada ya kucheza mchuano wa kirafiki siku ya Jumanne waliotoka sare ya mabao mawili kwa mawili.

Ujerumani ambao sasa wamesafiri na wachezaji 21 kwa mchuano huo wa kesho Jumapili mjini Tblisi, wamekuwa na mwanzo mbaya katika mechi za kufuzu, ambapo wamekusanya pointi saba katika michuano minne, mbele ya Ireland na Scotland, huku Poland ikiwa kileleni na pengo la pointi tatu katika Kundi D.

Mlinda lango Manuel Neuer yuko katika hali nzuri baada ya kusubmbuliwa na maumivu ya goti. Nahodha Bastian Schweinsteiger, pia anatarajiwa kucheza. Wachezaji wengine muhimu waliopumzishwa katika Jumanne wakiwemo Jerome Boateng, Thomas Mueller na Mats Hummels, wanatarajiwa kujumuishwa katika kikosi cha kwanza.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/Reuters/DPA
Mhariri: Yusuf Saumu

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com