1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani sasa ina serikali mpya

Sekione Kitojo
15 Machi 2018

Wahariri wa magazeti ya Ujerumani wamejishughulisha zaidi na mzozo kati ya Uingereza na Urusi kuhusiana na shambulio la sumu dhidi ya jasusi wa zamani wa Urusi nchini Uingereza, na pia kuhusu serikali mpya ya Ujerumani.

https://p.dw.com/p/2uMdF
Deutschland Ernennung des neuen Bundeskabinetts
Picha: Reuters/F. Bensch

Mhariri wa  gazeti  la Rhein-Zeitung  la  mjini  Koblenz  anaandika kwamba uchaguzi mwingine  wa  majimbo utaonesha iwapo kile kinachoonekana  kuwa ni kuaminika  na  wananchi  kwa  muungano wa  vyama vya  kihafidhina  na  SPD kuunda  serikali kumefanikiwa. Mhariri  anaendelea.

Mtihani wa  kwanza  utakuwa  mnamo wakati  wa  kuelekea mwishoni  mwa  mwaka  huu katika  jimbo  la  Bavaria  na  kisha Hesse. Mwaka 2019 kutakuwa  na  mtihani  mwingine  wa uchaguzi wa  bunge  la  Ulaya  na  kisha  uchaguzi  katika  majimbo  matatu ya mashariki  mwa  Ujerumani. Hali  itakwenda  vizuri , iwapo  vyama ndugu  vya  CDU /CSU  pamoja  na  SPD  hadi  wakati  huo wataonesha  kile  walichofanikisha, kwamba  wametatua  matatizo ya  wananchi.

Bila  hivyo  inawezekana  katika  majimbo  ya  mashariki wapiga kura  watakimbilia  katika  chama  mbadala  kwa  Ujerumani  AfD.

Nae mhariri  wa  gazeti  la Hannoversche Allgemeine  la  mjini Hannover  anaandika  kwamba  Kansela Angela Merkel  na  waziri wa fedha Olaf Scholz sasa wana  nafasi , kupitia sera muafaka za kubana  matumizi  katika  sehemu  kubwa  ya  eneo  la  kati  nchini na kunyamazisha   kile kilichoonekana  kuwa  ni ukweli katika majadiliano  yaliyokuwapo  katika  miezi iliyopita. Mhariri  anaandika.

Kwa mfano ni mara  ngapi watu wamesikia  nchini  Ujerumani maneno  kama  "hali haiwezi  kuendelea hivi"  Kila  mwananchi anaiangalia  hali  hii  kwa  njia  tofauti.  Baadhi  yao  ambao wanaona  hali  ya  kiuchumi  kuwa  nzuri , wataendelea  kupiga  kura , linasema  kundi  linalochunguza  maoni  ya  wapiga  kura, ambao wanafikia  ni karibu  Wajerumani asilimia  60. Mtazamo  wa  wale wanaosema  tuendelea  hivyo  hivyo  kiukweli  wanasema  hivyo kwa  misingi  ya upatikanaji  tu wa mahitaji ambao ndio unaowavutia zaidi.

Mzozo kati ya Uingereza  na Urusi

Nalo gazeti la  General-Anzeiger  la  mjini  Bonn  linaandika kuhusiana  na  mzozo  kati  ya  Uingereza  na  Urusi  kufuatia shambulio  la  sumu dhidi  ya  jasusi  wa  zamani  wa  Urusi  nchini Uingereza. Mhariri  anaandika.

Pande  zote mbili zinapambana , nyuma lakini  kuna  hali  ya  kuigiza ya  kutisha  ambayo haieleweki. Shambulio  dhidi ya  jasusi  wa zamani  aliyeamua  mwaka 2010  kukimbia  kutoka  Urusi  haliingii akilini. Kitu  kigani  serikali  ya  Urusi  itakipata  kwa  kufanya shambulio  hilo, siku  chache  kabla  ya  uchaguzi  ambao  Putin anawania  nchini  Urusi? Kwa  upande  mwingine  Uingereza  inataka nini , kwa  kufanya tukio  hili ambalo si la  kweli  na  kuweka  hali  ya wasi  wasi  kati  ya  Uingereza  na  Urusi, kama  vile wanavyodai Warusi.? Hakuna, mhariri  anaandika. Hali  mpya  mbaya  ya uhusiano  baridi  kati ya  mashariki  na  magharibi  inaongezeka.

Mhariri  wa  gazeti  la Stuttgerter Nachrichten  akizungumzia  mzozo huo   kati  ya  Uingereza  na  Urusi anaandika  kwamba  Imegundulika hakuna  ushahidi uliokwisha  tolewa.Mhariri  anaandika:

Kwamba  waziri  mkuu  wa  Uingereza  Theresa  May ametoa  sauti, lakini  kwa  mara  ya  kwanza  ametoa  adhabu ya hovyo hovyo  hivi.

Na  hili  hata yeye  binafsi  analifahamu.  Kutokana  na  hali  ilivyo Uingereza  pia inabidi kuwashirikisha  pia  washirika. Hii inahusu Ujerumani  pamoja  na mataifa  mengine  ya  Umoja  wa  Ulaya   na washirika  wa  NATO.  Kuna  ishara ya  wazi  kwamba  wote  wako upande wa  Uingereza, bila  kujali  Brexit. Na utayari , wa  kuimarisha vikwazo , iwapo serikali  ya  Urusi  itagundulika  kuwa  nyuma  ya shambulizi  hilo.

 

Mwandishi: Sekione Kitojo / Inlandspresse

Mhariri: Daniel Gakuba