Ujerumani, Norway zaanza Kombe la Dunia kwa kishindo | Michezo | DW | 08.06.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Ujerumani, Norway zaanza Kombe la Dunia kwa kishindo

Mabingwa wa zamani Ujerumani na Norway walianza kampeni zao katika dimba la Kombe la Dunia la FIFA 2015 kwa kupata ushindi dhidi ya Cote d'ivoire na Thailand wanaoshiriki kwa mara ya kwanza

Wanawake wa Ujerumani waliwararua Cote d'ivoire 10 -0 baada ya Norway kuwachabanga Thailand 4-0 katika michuano ya ufunguzi ya kundi B mjini Ottawa.

Ujerumani, washindi wa 2003 na 2007 walifunga mabao matano katika kila kipindi cha mchezo dhidi ya Wa Cote d''ivoire ambao ndio wanaoorodheshwa katika nafasi ya 67 katika viwango vya FIFA ulimwenguni, ndio wa mwisho katika kinyang'anyiro hicho.

Ujerumani na Norway sasa watawania nafasi ya kwanza katika kundi lao siku ya ALhamisi, mjini Ottawa katika mchuano ambao ni marudio ya dimba la mataifa ya Ulaya mwaka wa 2013 ambapo Wajerumani waliibuka kidedea.

Katika mechi za leo Jumatatu za Kundi C, mabingwa watetezi Japan wataanza kazi dhidi ya Uswisi, wakati Cameroon na Equardor ambao wanashiriki kwa mara ya kwanza wakipambana mjini Vancouver.

Mjini Winnipeg, washindi makra mbili Marekani, watachuana na Australia wakati Sweden wakiangushana na miamba wa Afrika Nigeria katika Kundi D.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/AP/reuters
Mhariri: Yusuf Saumu