Ujerumani na Uholanzi kuumana tena katika Euro 2020 | Michezo | DW | 03.12.2018
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Ujerumani na Uholanzi kuumana tena katika Euro 2020

Ujerumani kukumbana tena na Uholanzi katika michuano ya kufuzu kucheza fainali za Euro,

Ujerumani  na  Uholanzi  hazitaki  kuachana. walicheza  pamoja katika  ligi  ya  mataifa  ya  ulaya, na  sasa  tena  tutapata  michezo miwili  mikubwa  katika  kundi C.

UEFA Euro 2020 (Reuters/C. Kilcoyne)

Upangaji wa makundi ya kombe la Euro 2020 mjini Dublin

Kwa  upande  wa  kandanda la  kimataifa,  mabingwa  wa  zamani wa  kombe  la  Ulaya  Ujerumani  watapambana  na  Uholanzi  tena katika  kinyang'anyiro  cha  kuwania  kufuzu  kwa  ajili  ya  fainali  za Euro 2020  baada  ya  kuwekwa  pamoja  katika  upangaji  wa makundi  mjini  Dublin, lakini  Uingereza  iliyofikia  nusu  fainali  ya kombe  la  dunia  mwaka  huu  haina  sababu  ya  kulalamika juu  ya hilo.

Ujerumani  ilikuwa  timu  hatari  zaidi  katika  chungu namba mbili  baad  ya  kushuka  kutoka  katika  kundi  la  timu  za  juu  la  ligi ya  mataifa,  kwa  sehemu  fulani  kutokana  na  kipigo  cha  mabao 3-0 dhidi  ya  Uholanzi mwezi  Oktoba.

UEFA Euro 2020 (Reuters/C. Kilcoyne)

Rais wa shirikisho la kandanda barani Ulaya Aleksander Ceferin(kushoto) na rais wa Ireland Michael D. Higgins (kulia)

Ujerumani  itaanza  kampeni yake  kwa  kusafiri  kwenda  Uholanzi Machi 24  mwakani  kabla  ya kuwa  wenyeji  wa  majirani  zao  hao Septemba  6. Huyu  hapa kocha  wa  uholanzi Ronald  Koeman.

"Ni ngumu, inafurahisha kuwa  na  Ujerumani  katika  kundi  moja. Timu  ngumu  kabisa  katika  chungu  cha  pili  lakini  sawa tu tulicheza  dhidi  yao  wakati  huo  na  tunawajua  na  wanatujua na nafikiri  mengine  katika  kundi  hili yankubalika  na  naangalia matokeo  ya  kupangwa  katika  kundi  hili kwa  matumaini makubwa."

Kundi C

Ireland  ya  kaskazini, Estonia  na  Belarus  ni  timu  nyingine zenye jukumu  la  kuleta  mshangao  katika  kundi  la  C. Hata  hivyo  timu mbili  za  juu  katika  kila  kundi  katika  makundi  haya  10 zitaingia moja  kwa  moja  katika  kinyang'anyiro  cha  fainali  zitakazokuwa na  timu  24, ambazo zitachezwa  kwa  mara  ya  kwanza  katika  nchi 12  wenyeji,  hakuna  shaka  kwamba  mataifa  makubwa  vigogo  wa soka  la  Ulaya  yatakuwapo katika  fainali  hizo.

Deutschland | Reinhard Grindel präsentitert das UEFA Euro 2020 Logo (Getty Images/Bongarts/A. Beier)

Rais wa shirikisho la soka nchini Ujerumani Reinhard Grindel akionesha nembo ya UEFA

kundi  hili  ni  gumu,"  amesema  kocha  wa  Ujerumani  Joachim Loew, ambaye  yuko  chini  ya  mbinyo  akitakiwa  kuirejesha  timu yake  katika  nafasi  yake  baada  ya  kuanguka  katika  awamu  ya makundi  katika  kombe  la  dunia.

Hakuna sababu ya  kikosi  cha  kocha   Gareth Southgate  kuhofia katika  kundi  A kwa  kuwa  inaanza  na  mchezo  wa  nyumbani  dhidi ya  Jamhuri  ya  Cheki Machi 22, ambapo pia  England  inakumbana na  Bulgaria  , Montenegro  na  Kosovo. Kocha  gareth  Southgate:

"Kwa  hakika  kuna  nchi  ambazo  tungepangwa  nazo ambazo tumeepuka kama  Ujerumani  katika  chungu  cha  pili  na  serbia pamoja  na  nyingine  kadhaa  katika  chungu  namba  3, lakini tunashauku  kubwa  kufikia  fainali  hizi na  moja  kati  ya   miji wenyeji. Sisi  ni  moja  ya  miji  wenyeji, kwa  hiyo  tunahitaji  kuwa na  uhakika  wa  kufikia  huko."

 

Mwandishi: Sekione  Kitojo / afpe / dpae / rtre / ape

Mhariri: Mohammed Khelef