1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani na Ufaransa wazungumzia mkopo wa Ireland

Kabogo, Grace Patricia26 Novemba 2010

Nchi hizo mbili zinataka kuwepo hitimisho la haraka katika majadiliano ya kuinusuru Ireland.

https://p.dw.com/p/QIkX
Rais wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy, akiwa na Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel.Picha: AP

Ujerumani na Ufaransa zinataka kuona hitimisho la haraka la majadiliano kuhusu kuinusuru Ireland kiuchumi. Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel na Rais Nicolas Sarkozy wa Ufaransa, walizungumza kwa njia ya simu hapo jana, wakisema kuwa wamefurahishwa na hatua za kubana matumizi zilizotangazwa na serikali ya Ireland.

Hatua hizo ni masharti ya mwanzo iliyopewa Ireland ili iweze kupatiwa mkopo wa fedha na Umoja wa Ulaya na Shirika la Fedha la Kimataifa-IMF, ambao unakadiriwa kuwa na thamani ya Euro bilioni 85.

Kansela Merkel anashirikiana na Rais Sarkozy kuwasilisha pendekezo la kuwepo utaratibu wa kudumu kwa ajili ya kushughulika na mataifa ya Umoja wa Ulaya wakati yanapokabiliwa na matatizo ya kiuchumi.

Kansela Merkel na Rais Sarkozy wamekubaliana kwamba kiasi cha Euro bilioni 750 kilichopo sasa kwa ajili ya mpango wa kuyanusuru mataifa yanayotumia sarafu ya Euro, kinapaswa kubakia hivyo hadi mwaka 2013.

Mwandishi:Patricia Kabogo

Mpitiaji:Hamidou Oummilkheir