1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani na Finland leo

9 Septemba 2008

Katika kinyanganyiro cha kuania tiketi za kucheza kombe la dunia 2010 Ujerumani ina miadi jumatano na Finland.

https://p.dw.com/p/FEhZ
Katrin Green ashinda dhahabuPicha: picture-alliance/dpa

Wakati michezo ya olimpik ya walemavu(paralympics) ikiendelea mjini Beijing, macho ya mashabiki wa kabumbu ulimwenguni yanakodolewa changamoto mbali mbali za kukata tiketi kwa kombe lijalo la dunia nchini Afrika kusini 2010.

Ujerumani ina miadi leo na Finland huku Rais wa Shirikisho la dimba la Ujerumani Theo Zwanziger akitoa mwito kumalizwa ugomvi uliopo kati ya nahodha wa Ujerumani Michael Ballack na meneja wa timu ya Taifa Oliver Bierhof.

►◄

Ujerumani leo inakabiliwa na changamoto kali katika kiu chake cha kukata na mapema tikezi ya kucheza kombe lijalo la dunia huko Afrika Kusini.Mahasimu wao leo katika kundi lao la 4 sio Lichtenstein,walioizaba mabao 6 :0 mwishoni mwa wiki, bali Finland tena nyumbani mwao Helsinki.Kocha wa Ujerumani Joachim Loew anatazamiwa kuteremsha timu ile ile iliotimua nje Lichtenstein jumamosi. Hii ina maana hujuma za Ujerumani langoni mwa Finland zitaongozwa na washambulizi 2 wa klabu bingwa Bayern Munich-nao ni Lukas podolski alietia juzi mabao 2 na Miroslav Klose alietoka mikono mitupu.Inatarajiwa kwamba Miroslav Klose atauona leo wavu baada ya kitambo kirefu.

Ujerumani mabingwa mara 3 wa dunia na makamo-bingwa wa Ulaya wana rekodi nzuri mbele ya Finland katika mapambano 20 wameshindwa mara moja tu na Finland na ikiwa 1923.

Hizo lakini zilikua zama za zama,mapambano yao 2 yaliopita katika kufuzuku kwa kombe la dunia 2001 walitoka sare mara 2.Matokeo yake Ujerumani ilibidi icheze na Ukraine ili kunyakua tiketi yake ya kombe la dunia la 2002.

Mpambano huu unachezwa huku bado pakiwapo mvutano kati ya nahodha wa timu ya Ujerumani michael ballack alieumia na meneja wa timu ya taifa Oliver Bierhoff.Ugomvi kati yao ulianza tangupale Ujerumani ikiongozwa na ballack iliposhindwa kwa bao 1 na Spian katika finali ya kombe la Ulaya mjini Vienna,Juni mwaka huu.

Katika kanda ya Afrika Sudan leo ina miadi na Chad katika changamoto ya kundi la 10 wakati lile la 11 linazipambanisha leo Zambia na Togo.

Wakati Brazil na Bolivia na Argentina na Peru wana miadi kesho katika kanda ya Amerika kusini,leo ni zamu ya Paraguay kucheza na Venezuela wakati Uruguay wakipambana na Ecuador .Chile inacheza na Columbia.

Katika kanda ya bara la Asia,Uzbekistan inacheza leo na Australia huku Bahrein ikikutana na Qatar katika mapambano ya timu A.Kundi B linazileta uwanjani Korea ya kaskazini kucheza na ndugu zao wa kusini huku Umoja wa Falme za kiarabu ukiwa na miadi ma Saudi Arabia.

Katika medani ya paralympics-michezo ya olimpik kwa walemavu,chipukizi wa Poland Natalia Partyka ni mmoja kati ya wanariadha wachache sana waliomudu kushiriki michezo yote 2 ya olimpik- ile ya walemavu na ya sio-walemavu.Pia amefaulu kufanya kile wengine wameshindwa-kuwashinda machina katika "ping pong"-tennis ya mezani.Msichana huyo mwenye umri wa miaka 19, aliwahi pia kushiriki katika michezo ya walemavu ya olimpik ya Sydney,2000 akiwa na umri wa miaka 11 na miaka 4 baadae, akashinda medali yadhahabu huko Athens,Ugiriki.Natalia Partyka anaweka matarajio ya medali nyengine kutoka Beijing.