Ujerumani na England leo uwanjani | Michezo | DW | 18.11.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Ujerumani na England leo uwanjani

Timu hizo mbili hasimu zapambana leo huko Berlin kuoneshana dimba.

Kocha Loew na Ballack

Kocha Loew na Ballack

Leo timu kadhaa za kitaifa zinaingia uwanjani kwa changamoto za kirafiki:wakati Tanzania (Taifa Stars) ina miadi leo mjini Dar-es-salaam na jirani zao Msumbiji ili kulipiza kisasi kwa pigo la mara iliopita, Ujerumani ina miadi na England au Uingereza katika uwanja wa Olimpik wa Berlin. Timu zote mbili zitaingiza wachezaji wapya ama kwa kuumia wengine au kwa kuwajaribu hao wapya:

Mechi hii ya kirafiki inayokumbusha kila mara finali ya kombe la dunia ya 1966 uwanjani Wembley, inachezwa katika uwanja wa olimpik wa Berlin.Inachezwa huku taarifa ikichomoza kuwa kila mchezaji wa Ujerumani atalipwa kitita cha Euro laki 200.000 ikiwa Ujerumani itafaulu kukata tiketi ya kombe lijalo la dunia 2010 nchini Afrika kusini-la kwan za barani Afrika.

Mchezaji wa kiungo wa Schalke Jermaine Jones ni miongoni mwa chipukizi wapya watakao vaa jazi ya Ujerumani jioni hii huko Berlin tena kwa mara ya kwanza.Jones atnajaza pengo la Torsten Frings aliepigwa kumbo.Huo utakuwa mpambano wa kwanza kwa mtoto huyo wa mwanajeshi-mweusi wa kimarekani ,mzaliwa wa Ujerumani na aliekulia Frankfurt.Nahodha Michael Ballack akiwa hatakuwa uwanjani, jones aweza kucheza pamoja na Simon Rolfes wa viongozi wa Ligi-Bayer Leverkusen kutamba kati ya uwanja .Lukas Podolski,ambae hapati nafasi za kutosha kuichezea Bayern Munich, anatazamiwa kutamba kwa timu ya Taifa kama kawaida yake.

Kocha wa Uingereza ,mtaliana Fabio Capello nae anateremsha timu yenye sura mpya -kufuatia kuumia kwa wachezaji wake wengi: Steve Gerrad,Frank Lampard,Wyne Rooney,Wevs Brown,Rio Ferdinand na hata mastadi wa Chelsea wengine kama Ashley na Joe Cole.Hata mshambulizi Emile Heskey wako nje ya chaki ya uwanja kwa kuumia.

Wachezaji wapya kabisa wanaovaa leo jazi ya England ni pamoja na mlinzi wa Chelsea ,Michael Mancienne,alieazimwa sasa kwa Wolves na wachezaji 2 wa Aston villa Gabriel na Davies.

Ujerumani haikuwika mbele ya Uingereza katika mechi 7 zilizochezwa Berlin ba mara ya mwisho madume hawa 2 kukutana katika ardhi ya Ujerumani ,England ilitamba huko Munich kwa mabao 5-1,Septemba 2001.

Hatahivyo, Ujerumani imekuwa ikitamba karibuni pale timu hizi mbili zilipopambana .Ujerumani ilishuinda England mabao 2-1 uwanjani Wembley hapo August mwaka jana.

Kiasi cha mashabiki 10.000 wa Uingereza wanatazamiwa huko Berlin na vyombo vya usalama havina wasi wasi la kuzuka fujo.

Wachezaji 3 wapya kutoka klabu chipukizi ya Hoffeheim iliopanda msimu huu daraja ya kwanza na iko kileleni pamoja na Leverkusen pia wamechaguliwa katika kikosi cha leo.

Wachezaji wakongwe wa timu ya Taifa kama nahodha Michael Ballack na rafiki yake Torsten Frings walikorofishana na kocha Joachim Loew lakini bado maarufu katika timu hii.hata Philipp Lahm,beki mshahara,mchezaji wa kiungo Bastian Schweinsteiger na Simon Rolfes wana usemi mkubwa zaidi katika timu ya Ujerumani.

Kabla timu ya Ujerumani kuteremka leo jioni uwanjani, taarifa ilitoka kuwa kila mchezaji wa timu hiyo ya taifa atapewa kitita cha Euro laki 2 ikiwa Ujerumani itafuzu kukata tiketi ya kucheza kombe lijalo la dunia nchini Afrika kusini 2010.Wachezaji 4 wa usoni kabisa-nahodha Michael Ballack,Philip Lahm,Miroslav Klose na Torsten Frings ndio waliopatana na shirikisho la dimba la Ujerumani kwa kitita hicho.

Meneja wa timu ya Taifa Oliver Bierhoff,anasema mpango huo ulifikiwa baada ya mazungumzo ya dakika 40 tu.