1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uhusiano kati ya Ujerumani na China waimarika tena

21 Januari 2008
https://p.dw.com/p/CvQU

BERLIN.

Baada ya uhusiano kati ya Ujerumani na China kulegalega kwa miezi kadhaa,waziri mmoja wa china amesema kuwa kansela wa Ujerumani Angela Merkel anakaribishwa mjini Beijing. Akihojiwa na gazeti la kila siku la Ujerumani la Handelsblatt waziri wa sayansi na Teknolojia Wang Gang amesem akuwa China ina hamu ya kufanya majadialiano ya ngazi zote na Ujerumani. Uhusiano kati ya Ujerumani na China ulitiwa doa baada ya Merkel,mwezi wa Septemba, alipovunja daftari ya kihistoria kuwa kiongozi wa kwanza wa Ujerumani kumaribisha Dalai Lama.Mkutano wake na kiongozi wa Tibet alioko uhamishoni uliifanya China kuvunja mikutano kadhaa ya nchi hizi mbili.