Uhusiano kati ya Marekani n a Libya | IDHAA YA KISWAHILI | DW | 04.01.2008
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

IDHAA YA KISWAHILI

Uhusiano kati ya Marekani n a Libya

Waziri wa nje wa Libya Shalgam anazuru Marekani huku Libya ikichukua wadhifa wa mwenyekiti wa Baraza la Usalama.

Kwa kuingia mwaka mpya,Libya imekalia kiti cha mwenyekiti wa Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa mjini New York, kilele cha kurejea katika jukwaa la siasa za kimataifa na kuheshimika. Sambamba na tokeo hili,waziri wa nje wa Libya Mohammed Abdel-Rahman Shalgam anazuru Washington, ikiwa ziara adimu kabisa na ya kwanza kwa waziri wa nje wa Libya tangu 1972.Amekutana jana na waziri wa nje Dr.Condoleeza Rice ambae alizusha maswali ya ufumbuzi wa matatizo ya siku za nyuma,haki za binadamu nchini Libya na siasa za kilimwengu.

„Hatuzungumzi tena juu ya vita au mvutano au ugaidi,kinyume chake.Tunazungumzia utajiri wa watu wetu,ushirikiano,uwekezaji raslimali,amani na utulivu“-alisema waziri wa nje wa Libya baada ya kutia saini mapatano juu ya ushirikiano katika sekta ya elimu na ufundi.

Nae msemaji wa wizara ya nje ya Marekani, Sean McCormack

Amearifu kwamba waziri wa nje wa marekani dr.Condoleeza Rice, katika mazungumzo yake na waziri mwenzake wa mambo ya nje wa Libya Shalgam, alizusha maswali kama ufumbuzi wa matatizo ya zamani,haki za binadamu na ya siasa za kimataifa.

Dr.Rice aliitaka Libya kusonga mbele kusuluhisha madai yaliosalia ya jamaa wa wahanga wa shambulio la ndege ya Pan Am huko Lockerby,Scotland na kukanyagwa kwa haki za binadamu nchini Libya.

Mahusiano kati ya Washington na Tripoli yamechangamka tangu pale Libya kuacha kuungamkono kile Marekani inachokiita „Ugaidi wa kimataifa“ pamoja pia na kukomesha mradi wake wa kinuklia hapo 2003 –hatua ambayo Marekani imekuwa pia ikiishawishi Korea ya kaskazini na nchi nyengine kuiga.

Uhusiano huu lakini umezorota kutokana na kutosuluhishwa kikamilifu mpango wa malipo ya fidia kwa jamaa wa wahanga

wa Lockerby pamoja na wale wa shambulio la Disco mjini berlin,Ujerumani.Wamarekani waliuwawa katika njama zote hizo 2.

Libya ilijitwika jukumu la kulipa fidia kwa kima cha dala milioni 10 kwa kila mhanga, lakini haikulipa bado malipo ya mwisho.Halkadhalika, haikulipa bado fidia kwa jamaa wa wahanga wa Marekani wa shambulio la Disco la La Belle huko Berlin magharibi.

Seneta Robert Mendez wa chama cha Democrat nchini Marekani ameikosoa utawala wa George Bush kukaa mezani na kula chakula na kunywa mvinyo“ na waziri wa nje wa Libya kabla mkasa wa Lockerby,haukupatiwa ufumbuzi kikamilifu.

Waziri wa nje wa Marekani Dr.Rice amesisitiza tena hapo jana azma yake ya kuitembelea Libya wakati muwafaka.

Ilikua Julai mwaka huu pale Libya ilipomaliza ule mvutano wa kibalozi ilipowaacha huru wauuguzi 5 wa kibulgaria na daktari 1 wa kipalestina waliokuwa kizuizini tangu 1999 kwa mashtaka ya kuwaambukiza virusi vya Ukimwi watoto wa Libya.

Marekani sasa inataka kushirikiana hata sasa kiti cha rais wa baraza la Usalama la UM kwa mwaka huu na hasa katika maswali kama vile Kosovo,Iran na Sudan-alisema dr.C.Rice.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com