Uhuru wa vyombo vya habari Ujerumani | Matukio ya Kisiasa | DW | 19.01.2011
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Uhuru wa vyombo vya habari Ujerumani

Uhuru wa vyombo vya habari una hadhi kubwa nchini Ujerumani na ni sehemu ya haki ya kimsingi inayodhaminiwa katika katiba ya nchi. Hiyo ndio nadharia, lakini matukio kadhaa yanazusha wasiwasi.

Puzzlebild Pressefreiheit 2 Unsere Arbeit ist mehr wert und Unser Land braucht seine Zeitungen steht auf Transparenten bei einer Protestkundgebung des Deutschen Journalisten-Verbandes (DJV) während des DJV-Bundesverbandstages 2008 am Mittwoch (05.11.2008) in Rostock. Seit Montag (03.11.2008) berieten die 300 Delegierten während des dreitägigen Treffens u.a. über die tarifpolitische Auseinandersetzung im Printbereich, über die Pressefreiheit und über die Zukunft des Journalistenberufs. Foto: Bernd Wüstneck dpa/lmv +++(c) dpa - Report+++

Waandishi wa habari wa Ujerumani wadai uhuru wa vyombo vya habari

Kwa mfano, mwaka 2005, ofisi za jarida la Cicero na nyumba ya mwandishi mmoja wa habari zilipekuliwa kwa mashtaka ya kusaidia kufichua siri. Hiyo ni sababu iliyotolewa na waendesha mashtaka wa serikali mjini Potsdam. Chanzo, ni ripoti iliyonukulu habari za siri kutoka idara kuu ya upelelezi wa uhalifu ya Ujerumani BKA. Mkasa huo wa Cicero si tukio pekee lililoshangaza hivi karibuni.

Kwa hivyo, wala si ajabu kuona kuwa Ujerumani imeshika nafasi ya 17 katika orodha mpya ya mwaka inayoshuika na uhuru wa vyombo vya habari. Orodha hiyo inatayarishwa na shirika la "Waandishi wasio na Mipaka". Shirika hilo liliundwa na waandishi wa habari mwaka 1985 nchini Ufaransa na linatetea haki za binadamu. Msemaji wa tawi la shirika hilo nchini Ujerumani katika mji mkuu Berlin ni Michael Rediske. Yeye anasema, wala hakushangazwa na orodha hiyo ya mpya na kuongezea.

"Mara kwa mara kinga ya wenye kutoa habari hukiukwa, huku ofisi za magazeti zikipekuliwa.Lakini hivi karibuni, mahakama kuu ya katiba imesema kuwa upekuzi uliofanywa katika kituo binafsi cha matangazo mjini Hamburg, ni kinyume na katiba."

Mambo yangekuwa mabaya zaidi bila ya mahakama kuu. Kwani mara nyingi, uamuzi wa mahakimu, unaunga mkono uhuru wa vyombo vya habari. Kwa mfano, uamuzi wa mahakama umepinga sheria iliyotaka kuruhusu kwa masharti maalum, kuchunguza kwa siri, tovuti za watu binafsi.

Pengo lazidi kati ya vyombo vya habari na serikali

Mit ihrem Vorsitzenden Michael Konken (M) an der Spitze demonstrieren am Dienstag (06.11.2007) in Saarbrücken die Teilnehmer des Bundestages des Deutschen Journalistenverbandes für Pressefreiheit. Kurz vor der Entscheidung des Bundestags über die umstrittene Vorratsdatenspeicherung hat der Deutsche Journalisten-Verband (DJV) vor katastrophalen Folgen für die Pressefreiheit gewarnt. Foto: Becker & Bredel dpa/lrs (zu lrs 7411 vom 06.11.2007) +++(c) dpa - Bildfunk+++

Mwenyekiti wa DJV, Michael Konken(katikati) akiongoza maandamano

Wakati huo huo, Michael Konken alie mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari nchini Ujerumani DJV anaamini kuwa tangu miaka kadhaa, mwanya unazidi kuwa mkubwa kati ya vyombo vya habari na wanasiasa.Anasema:

" Uwezo wa kuwakosoa wanasiasa umetoweka, miaka hii iliyopita. Waandishi wa habari wanatazamwa kama ni maadui. Serikali inapaswa kuchukua hatua ili kuhakikisha uhuru wa vyombo vya habari na uhuru wa kuripoti."

Hata mazingira mabaya ya kiuchumi, yanaathiri uhuru wa vyombo vya habari. Nchini Ujerumani, ni makampuni kadhaa tu ndio yanayodhibiti sekta hiyo, kwa hivyo ni vigumu kuwepo maoni tofauti. Konken ana hofu kuwa uandishi wa habari hatimae huenda ikawa kazi inayofanywa na watu kama njia ya kujipatia vijisenti. Na hiyo haitokuwa kwa maslahi ya uhuru wa vyombo vya habari nchini Ujerumani.

Mwandishi:Fürstenau,Marcel /ZR/Martin,Prema

Mpitiaji:Abdul-Rahman,Mohammed

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com