Uhondo wa Ligi ya Premier ya England warejea | Michezo | DW | 10.08.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Michezo

Uhondo wa Ligi ya Premier ya England warejea

Msimu mpya wa ligi kuu ya kandanda England ulirejea tena mwishoni mwa wiki ambapo mashabiki walipata fursa ya kuzikaribisha timu zao wakiwa na matumaini makubwa

Lakini kuna wale waliopata mshangao mkubwa na namna mambo yalivyoanza. Mabingwa watetezi Chelsea walimudu tu kupata sare ya mbili mbili nyumbani dhidi ya Swansea wakati mlinda mlango wao Thibaut Courtois akilambishwa kadi nyekundu maana kuwa atakosa mchuano muhimu ujao dhidi ya Manchester City ugenini.

Mlinda mlango mpya wa Arsenal ambaye alipokonywa nafasi na Courtois katika klabu ya Chelsea, Petr Cech alifanya makosa mawili wakati Arsenal ikiduwazwa na West Ham nyumbani mbili bila.

Manchester United ilihitaji bao la kujifunga lake Kyle Walker ili kupata ushindi wa goli moja kwa bila dhidi ya Tottenham Hotspur. Philippe Coutinho alifunga bao safi katika dakika za mwisho mwisho na kuipa Liverpool ushindi wa moja bila dhidi ya Stoke City.

Watford ilitoka sare ya mbili mbili na Everton wakati Bournemouth ikifungwa moja bila na Aston Villa. Norwich City ilizabwa tatu moja dhidi ya Crystal Palace. Hii leo Manchester City watachuana na West Bromwich Albion.

Mwandishi: Bruce Amani/AFP/DPA/AP/reuters
Mhariri: Mohammed Khelef