1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uholanzi mabingwa wa Ulaya

Sekione Kitojo
7 Agosti 2017

Fainali  ya  kombe  la  ubingwa wa Ulaya  kwa kandanda la  Wanawake  nchini  Uholanzi  iliyoshuhudia  mabao  sita yakitinga  wavuni , ilikuwa  chachu nzuri katika michuano hiyo na kuipa kandanda  la  wanawake umaaufu.

https://p.dw.com/p/2hq2q
Fussball Europameisterschaft der Frauen 2017 Niderlande vs Schweden
Picha: Getty Images/D. Mouhtaropoulos

Ni nguvu  kubwa   ya mchezo  huo  sasa  inayozidi  kukua  katika  bara hilo, kwa  kuhudhuriwa  na  mashabiki  wengi  pamoja  na kupata idadi  kubwa  ya  watu  waliokuwa  wakiangalia katika  televisheni.

Idadi  iliyoongezeka  ya  timu  zilizoshiriki   kufikia  16 kutoka  12  za  hapo  awali  ilipandisha uhudhuriaji  kufikia hadi  watu  240,000  katika  michezo  31,  ikiwa  ni  juu kuliko  ilivyokuwa  miaka  minne  iliyopita  ambapo waliohudhuria  walifikia  217,000, wakati  ambapo  michezo yote  ya  mabingwa  wa  mashindano  hayo  Uholanzi  tikiti zake  zote zikiwa  ziliuzwa.

Fussball Europameisterschaft der Frauen 2017 Niderlande vs Schweden
Wachezaji wa Uholanzi wakishangiria ushindiPicha: Getty Images/D. Mouhtaropoulos

Uholanzi  iliishinda Denmark  kwa  mabao 4-2 na  kocha wa  Uholanzi  alisema Denmark  pia  walicheza  kandanda safi  ya  ushindani.

"Kulikuwa  na  timu  mbili ambazo  zilitaka  kucheza kandanda, kucheza  mchezo  wa  kumiliki  mpira na  kutaka hasa  kushinda , licha  ya  kwamba  ni  ukweli  usiofichika katika  fainali , lakini  mchezo ulioshuhudia  mabao  sita, tulikuwa  bora hata  hivyo, lakini  Denmark  pia  walionesha kwamba  wana  uwezo  mkubwa katika  fainali, Nadim , Harder , na  wengine  wote waliweka  mbinyo  mkubwa, kwa  hiyo  nafikiri  kwa  mashabiki  ilikuwa  jioni  nzuri na kwa  upande  wetu pia."

Fussball Europameisterschaft der Frauen 2017 Niderlande vs Schweden
Bao kwa Uholanzi na Denmark wanaliaPicha: Getty Images/AFP/D. Mihailescu

Viviane Miedema  alifunga  mabao  mawili wakati  wenyeji Uholanzi  wakiishinda  Denmark  kwa  mabao 4-2 jana Jumapili  na  kuwa  taifa  la  nne  kushinda  ubingwa  wa kandanda  la  wanawake  barani  Ulaya  tangu michezo hiyo  kuanza  mwaka  1984.

 

Mwandishi: Sekione Kitojo/dpae,afpe,rtre,ape

Mhariri: Mohammed Khelef