Uhariri wa magazeti ya Ujerumani. | Magazetini | DW | 16.04.2007
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Magazetini

Uhariri wa magazeti ya Ujerumani.

Sekione Kitojo amewakusanyia yale yaliyoandikwa katika magazeti ya Ujerumani hii leo, na wahariri wameshughulikia zaidi mada mbili muhimu. Maadhimisho ya miaka 80 ya kuzaliwa kiongozi wa kanisa Katoliki Papa Benedict wa 16 na pia hali nchini Russia. Gazeti la Badischen Neuesten Nachrichten kutoka Karlsruhe linazungumzia kuhusu mwaka wa 80 wa kuzaliwa kwa Papa Benedict wa 16. Gazeti hilo linaandika.

Kiongozi wa kanisa Katoliki Pop Benedict 16 atimiza miaka 80.

Kiongozi wa kanisa Katoliki Pop Benedict 16 atimiza miaka 80.

Hivi sasa anatimiza Joseph Ratzinger miaka miwili katika wadhifa huo wa Papa, kuna maamuzi ambayo hayaungwi mkono na watu wengi ambayo yako mbele yake, na pia anajaribu kudhibiti hali ya mizozo. Zaidi ya Wakatoliki bilioni moja duniani kote wanasubiri ishara kutoka Rome, kuhusiana na kuondolewa kwa mipaka ya kidini na kuhusu hilo wanaangalia tu mjini Rome.

Kunakuwa na hali hata hivyo hapa na pale ya kutokuwa na uvumilivu na kutoridhishwa. Pamoja na hayo Benedict anahitaji kutakiwa kila la kheri, kutokana na siku yake hii muhimu na watu wote kutoka kila pembe ya dunia.

Kwa maoni ya gazeti la Neuen Ruhr Zeitung Pop ameushangaza ulimwengu.

Baada ya kuchaguliwa gazeti hilo linaandika kuwa kulikuwa na masuala ya upendeleo, kuhusiana na masuala ya kisomi, kitamaduni na hata Ujerumani yenyewe. Benedict ameweka wazi kuanzia mwanzo wa kazi yake hiyo kama alivyojieleza binafsi. Yeye ni mfanyakazi wa kawaida wa watu, na hataendeshwa na vyombo vya habari au jamii ya vijana. Uamuzi kwa hiyo utakuja kwa muda aliopanga yeye.

Lakini gazeti la Braunschweiger linauliza:

Uamuzi wa hivi karibuni kabisa kwa ajili ya misa zinazosomwa kwa Kilatini , pamoja na msimamo wake mkali ambao haubadiliki kuhusiana na ishara ya kutenga mambo ya kiroho. Pop huyu linaandika gazeti hili kuwa anataka kuliweka kanisa mbali na dunia hii. Kanisa kama anavyolifahamu Benedict ni eneo la kiutawala, ambalo ni sehemu takatifu.

Iko sehemu ambayo iko wazi lakini haiwezi kufunguka zaidi ya hapo. Hali ambayo ni ngumu kwa mtu wa nje, lakini yule aliyeko ndani ni sehemu ambayo haipaswi kuingiliwa.

Hali nchini Russia ni suala pia ambalo limeshughulikiwa na wahariri wa magazeti ya leo. Gazeti la Frankfurter Allgemeine Zeitung likiandika kuhusiana na hali nchini Russia baada ya polisi kupambana na waandamanaji linasema.

Waandamanaji walipambana na polisi wa dola na wengine kukamatwa, pamoja na kwamba walikuwa si zaidi ya mia moja. Ni wazi kwamba utawala wote wa kisiasa , ambao rais wa Russia amekuwa kwa muda wote akiutumia kuwakandamiza, hivi sasa hauna uwezo wa kufanya hivyo tena

. Kama vile ambavyo bara la Ulaya , lingependa kuwa na uhusiano muhimu wa ushirika na Russia, haliwezi tena kuacha mambo kama yalivyo.

Nalo gazeti la Süddeutsche Zeitung linauliza sababu ya mapambano hayo na polisi.

Jibu linaweza kuwa katika mambo mawili kwanza ni hofu. Kila mmoja katika watawala wa Moscow wanaogopana na wanataka kulipanua suala hili. Russia inatakiwa kutawaliwa kwa njia ya kuwa na kikosi cha upelelezi kama zamani , kukiwa na hali ya kutokuaminiana pamoja na udhibiti wa utawala wa nchi. Kutokana na hali hii utawala wa Russia umekuwa ukifanyakazi zake bila ya utaalamu wa kutosha, na kuukandamiza upinzani. Wapinzani wa Putin wanaonekana kama wahalifu, wakati mfumo wa udhibiti ukitafutiwa hoja ya kuwa halali kwa kutafuta adui wa ndani.

Katika mataifa ya magharibi hali hii inaleta mshangao mkubwa.

 • Tarehe 16.04.2007
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CHTE
 • Tarehe 16.04.2007
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CHTE