Ugumu wa safari ya wakimbizi kuja Ulaya | Masuala ya Jamii | DW | 01.09.2015
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages
Matangazo

Masuala ya Jamii

Ugumu wa safari ya wakimbizi kuja Ulaya

Kila siku maelfu ya wakimbizi wanasafari wakijaribu kuingia nchi za Umoja wa Ulaya. Katika kipindi cha Mwangaza wa Ulaya tunakutana na wakimbizi, askari wa kulinda mipaka na watu wanaotoa misaada.

Macedonia si miongoni mwa nchi maarufu duniani. Lakini katika siku za hivi karibuni imekuwa ikigonga vichwa vya habari mara kwa mara kwa sababu ni moja ya nchi ambazo wakimbizi wanazipitia wakitaka kuingia katika Umoja wa Ulaya. Inakadiriwa kwamba zaidi ya wahamiaji laki moja wamefunga safari kutokea Ugiriki na kwenda Macedonia, Serbia na baadae Hungary katika juhudi za kupata hifadhi.

Mwandishi wa DW Nemanja Rujevic ameambatana na wakimbizi hao na kusikia visa vyao katika safari ndefu ya kukimbia vita na adha huko wanakotokea. Simulizi yake mnaletewa na Elizabeth Shoo katika Mwangaza wa Ulaya.

Kusikiliza kipindi bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.

Sauti na Vidio Kuhusu Mada

Matangazo

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com