Ugiriki haina budi kukaza mkaja | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 30.04.2010
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Ugiriki haina budi kukaza mkaja

Ugiriki haina budi ila kuchukua hatua kali zaidi kupunguza nakisi kubwa iliyopo katika bajeti yake ili iweze kujinusuru kwenda muflis.

Prime Minister George Papandreou speaks to reporters after meeting President Karolos Papoulias in central Athens, Greece, on Wednesday, March 3, 2010. Papandreou's Socialist government announced painful new austerity measures Wednesday worth euro4.8 billion ($6.5 billion) in savings to deal with an unprecedented financial crisis that has hammered the euro and driven up Greece's cost of borrowing. (AP Photo/Petros Giannakouris)

Waziri Mkuu wa Ugiriki, George Papandreou.

Kuambatana na masharti ya msaada wa kimataifa wa mabilioni ya Euro, hatua zinazopaswa kuchukuliwa ni kupunguza mishahara na nafasi za ajira serikalini, kutotoa nyongeza ya mishahara kwa angalao miaka mitatu ijayo,kupandisha kodi ya mapato na mauzo. Hiyo imetangazwa kufuatia mkutano wa dharura uliofanywa mjini Athens kati ya Waziri Mkuu George Papandreou na vyama vya wafanyakazi na wafanyabiashara. Hatua hizo zinapingwa vikali na wananchi wengi na hiyo jana, ghasia zilizuka mjini Athens. Polisi ilitumia gesi ya kutoa machozi kuwatawanya waandamanaji waliojaribu kuvamia jengo la wizara ya fedha.

Mpango huo wa kukaza mkaja, huenda ukawa mfano wa kufuatwa na nchi zingine za Ulaya ambazo vile vile zinapambana na matatizo makubwa ya deni. Kwani baada ya Ureno na Uhispania kuorodheshwa kama nchi zisizo na uwezo mzuri wa kulipa madeni yake, serikali za nchi hizo zinajitahidi kurejesha imani katika masoko ya fedha.

Mwandishi:P.Martin/DPA

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com