1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uganda yatakiwa kufanya uchunguzi wa shambulio

Sekione Kitojo
27 Novemba 2018

Uganda imetakiwa kuchunguza shambulizi la kijeshi lililofanywa dhidi ya makao ya mfalme miaka miwili iliyopita na watu 100 waliuawa.

https://p.dw.com/p/38yFa
Uganda Kampala Armee Major General Peter Elwel
Picha: DW/E. Lubega

Marekani na mataifa mengine wanawataka maafisa wa Uganda kuchunguza kwa ukamilifu shambulio la kijeshi dhidi ya makao  ya  mfalme miaka miwili iliyopita ambapo raia 100 waliuwawa na hatua hiyo ilishutumiwa kwa kiasi kikubwa. 

Kiasi ya watoto 15 walikuwa miongoni mwa wahanga wa shambulio hilo la Novemba 2016 lililolenga ufalme huo unaofahamika kama  Rwenzururu, ambao kiongozi wake kwa miaka kadhaa alikuwa anapinga utawala wa kiongozi wa muda mrefu wa Uganda Yoweri Museveni, kwa mujibu wa shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch.

Mauaji hayo yanafuatia mapigano kati ya polisi na wafuasi wa mfalme huyo wa kikabila, ambaye baadaye alikamatwa na kufunguliwa  mashitaka pamoja na mamia ya wafuasi wake. Wengi bado wako kizuwizini.