Uganda yapambana kuondoa matatizo ya umeme. | Matukio ya Kisiasa | DW | 28.07.2007
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Uganda yapambana kuondoa matatizo ya umeme.

Maji pamoja na jua vinapatikana kwa wingi . Hali kwa kuangalia tu nchini Uganda inaonekana kuwa bora katika matumizi mapya ya nishati ili kuzalisha umeme kwa mahitaji ya nchi hiyo. Lakini hata hivyo ukweli halisi unaonekana vingine. Kwa muda wa miaka mingi sasa kumekuwa na upungufu mkubwa wa nishati, hali ambayo inaleta athari katika uchumi na kusababisha maendeleo duni kwa jumla katika nchi ya Uganda. Maelezo haya yaliyoandikwa na Marcel Fürstenau.

Mashine zinafanyakazi, mikanda ambayo haionekani mwisho wake inatoa biskuti zilizookwa vizuri, na kando yake kuna akina mama ambao wanazimbua na kuzipanga hara haraka katika makasha ya gramu 200 ambayo hatimaye yanasafirishwa kwenda kwa walaji. Bila matatizo uzalishaji unaendelea katika kiwanda hiki cha Britania katika eneo la Ntinda lililopo karibu na eneo la kuingia katika mji mkuu Kampala. Kampuni hii ambayo pia inazalisha juisi ya matunda pamoja na pipi, mara kwa mara hukumbwa na matatizo ya kukosa umeme.

Mkuu wa uzalishaji Rafael Kimoni huwa na wasi wasi kila wakati.

Kutokana na kukatika mara kwa mara kwa umeme hatuwezi kufikia malengo yetu ya kibiashara. Tunahitaji kwa mfano kuzalisha tani 2,000 za biskuti kwa mwezi. Lakini katika mwezi wa May pekee tumepoteza siku 11 za uzalishaji. Kwa hiyo kufikia lengo letu inakuwa ni vigumu sana.

Matumaini ya kuimarika kwa hali katika uzalishaji wa biskuti pamoja na juisi katika kiwanda hiki cha Britannia , inaweza kupatikana katika mradi unaojulikana kama Bujagali. Hili ni jina la mradi wa umeme unaozalishwa kwa maji, ambao tayari unajengwa katika mto Nile unaotoka katika ziwa Victoria ukipata usaidizi kutoka serikali ya Ujerumani. Mradi huu unagharimu kiasi cha dola za Marekani 760, ambao utakamilika katika muda wa miaka minne na utaweza kuzalisha kiasi cha megawati 250 za umeme. Asilimia 80 ya fedha hizo zinatoka katika benki ya maendeleo ya kimataifa , inayotoa mikopo kwa ajili ya ujenzi mpya.

Nguvu za maji haya ya mto Nile kutoka katika ziwa Viktoria tayari zinatoa umeme kuanzia mwaka 1954. Wakati huo kinu cha Nalubaale kilikamilika kujengwa. Pamoja na kituo kingine kilichokuja jengwa baadaye cha Kiira , kwa juma vilikuwa na uwezo wa kuzalisha kiasi cha megawati 380 za umeme na kwa hiyo kukidhi mahitaji yote ya umeme nchini Uganda ikiwa na jumla ya wakaazi milioni 27 wakati huo. Kwa kulinganisha umeme kiasi hicho unahitajika kwa mji wa ukubwa wa kati kama Bochum ukiwa na wakaazi 375,000 nchini Ujerumani. Ikilinganishwa hata hivyo pia na mahitaji madogo nchini Uganda.

Uzalishaji hata hivyo ulianza nchini Uganda kwa kiasi cha megawat 120 tu ikiwa ni robo tatu tu ya uwezo huo wa megawat 380. Kufuatia miaka kadha ya ukame, kiwango cha maji katika ziwa Viktoria kilipungua kwa karibu mita mbili. Kutokana na kinu cha kisasa kabisa cha Bujagali cha kuzalisha umeme, inaonyesha juhudi sahihi za kirafiki na kuwa ni jambo zuri sana , kama anavyoamini msemaji wa mradi huo Jimmy Kiberu

Kinu hiki cha umeme ni nafasi ya kuonyesha uwezo wa Uganda kwamba inaweza kuwa moja kati ya nguvu kuu za uzalishaji wa umeme. Na wakati kutakapokuwa na viwanda vingi, itakuwa chanzo cha umasikini kupungua.

Na kwa hiyo athari zitakazopatikana kupitia usalama wa nishati kwa ajili ya viwanda kwa upande huo itakuwa kubwa.

Uwezo wake mradi huu wa Bujagali utaonekana , wakati kazi ya uzalishaji itakapoanza. Kwa sasa watu nchini Uganda wataendelea kuishi na matatuzo makubwa ya umeme. Katika kiwanda cha biskuti na juisi cha Britannia kilichoko mwendo wa saa moja tu kutoka mjini Kampala, mkuu wa uzalishaji Rafael Kimoni ataendelea kupata matatizo ya kukatika kwa umeme kwa muda wa miaka michache ijayo na kwa hiyo ataendelea kutegemea genereta ya kuzalisha umeme kiwandani hayo na hii inamaa matumizi zaidi ya fedha. Anasema kuwa wakitumia genereta kwa ajili ya kiwanda hicho , gharama zinapanda kwa zaidi ya mara nne.

 • Tarehe 28.07.2007
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CHAP
 • Tarehe 28.07.2007
 • Mwandishi Sekione Kitojo
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo https://p.dw.com/p/CHAP

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com